Ujumbe wa Viongozi wa dini wakiangalia mojawapo ya visima vya nchi kavu vya kusafisha gesi katika eneo la Mnazi Bay, Mtwara.
Viongozi
wa dini wametembelea Bomba Jipya la Gesi asilia la Mtwara- Dar es
Salaam, mtambo wa kusafisha umeme wa Mnazi Bay na maeneo mengine
mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na
Mtwara.
Viongozi
hao wamefanya ziara hiyo ikiwa ni maandalizi kabla ya kufanyika
Kongamano la Viongozi wa dini linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es
Salaam tarehe 21 na 22 mwezi Januari, 2014.
Viongozi
wa dini wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Masuala ya gesi na
Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya kusafisha gesi Mhandisi Sultan Pwaga
katika eneo la Madimba kinapojengwa Kiwanda cha kutakasa Gesi. Mafundi wa Kampuni ya China Petroleum Pipline (CPP) wakiendelea na kazi ya kuunganisha mambomba ya gesi katika kambi ya Madangwa.
Meneja
Mradi wa Bomba la gesi kutoka Da r es Salaam hadi Mtwara Mhandisi
Kapuulya Musomba akiwaeleza viongozi wa hatua mbalimbali zilizofikiwa
katika utekelezaji wa Mradi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini Mhandisi Ngosi MwihavaTUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIIII MOTOMOTO(USIPITWEEEEE)
No comments:
Post a Comment