Hii ni moja kati ya nyumba za polisi ambazo zimeharibiwa na mafuriko.
Hili ni eneo lililokumbwa na mafuriko hayo.
mafuriko yaliharibu vitu mbalimbali.
nyuma ya Askari polisi iliyobomolewa na maji.
Naibu waziri wa Nishati na Madini George B. Simbachawene (MB) akizungumza na wakazi wa Kijiji hicho.
Kamisha
msaidizi mwandamizi wa Polisi Daid Misime akiongea na wakazi wa kijiji
cha Chipogolo namna ya kuweka ulinzi kijijini hapo.
Kituo cha Polisi Chipogolo kilichobomolewa na mafuriko hayo.
SGT SOTELI wa jeshi la polisi kituo cha polisi Chipogolo ambaye pia ni muathirika wa Mafuriko hayo akifafanua jambo kwa Kamanda.
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma .
Kufuatia
mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma, nyumba 127
zimebomolewa na mafuriko ambapo watu 493 wamekosa makazi ya kuishi, pia
nyumba 240 zimezingirwa na maji katika Kijiji cha Chipogolo Kata ya
Chipogolo Tarafa ya Rudi Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma na kusababisha
jumla ya wakazi 1390 kukosa makazi ya kuishi.
Akiongea
na wakazi wa Kijiji hicho Naibu Waziri wa Nishati na madini ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa Mh. George Boniface
SimbaChawene amesema katika kikao cha tathmini kilichofanyika mara baada
ya kukagua eneo lililoathilika na mafuriko wamekubaliana kuwa hatua
mbalimbali zichukuliwe ikiwemo kujenga upya madaraja yaliyopo pamoja na
kuongeza kimo na urefu wa madaraja hayo kwa kuwa madaraja yaliyopo ni
mafupi na yanazidiwa na maji jambo ambalo linapelekea maji hayo
kushindwa kupita kwenye madaraja hayo na kuelekea kwenye makazi ya watu.
Pia
Mbunge huyo ameiomba kamati ya maafa kufanya kila liwezekanalo
kuhakikisha kwamba wakazi wa kijiji hicho wanapata huduma mbalimbali
zikiwemo za Afya kwa kuwapa madawa, elimu pamoja na kuwaongezea
wataalamu wa afya, kuwapatia Mahema, mablaketi na magodoro na chakula.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Christopher Ryoba Kangoye
amewaomba wakazi wa kijiji hicho kuendelea kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki kigumu wakati serikali kupitia kamati ya maafa Mkoa wa
Dodoma ikiendelea kushughulikias matatizo yao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David
A. Misime amewataadharisha wakazi wa kijiji hicho kuwa watulivu kwani
matatizo kama haya hayatatuliwi kwa vurugu badala yake watumie vikao
vinavyostahili kutatua matatizo yao “matatizo kama haya hayatatuliwi kwa
kufanya fujo na kufunga barabara”
Wakati
huohuo Kituo cha Polisi Kata ya Chipogolo na nyumba tano za Askari wa
kituo hicho zimeanguka kutokana na mafuriko hayo, Kamanda Misime ametoa
pole kwa Askari wa kituo hicho na kuwasisitiza waendelee kufanya kazi
kwa maadili ya Jeshi bila kujali wakati tatizo lao linashughulikiwa na
mamlaka husika kwani vituo vya Polisi kama hivyo vipo chini ya
Mkurugenzi na wananchi kwakuwa vilijengwa kwa nguvu zao.
michuzi blog
No comments:
Post a Comment