Na Kibada Kibada-Mpanda
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Kapt Mstaafu George Huruma
Mkukuchika amewataka watumishi wa umma na kila mmoja kwa nafasi yake
kuzingatia maadili ili kila katika utumishi wa umma ili kuimalisha
utendaji na kuepuka vitendo vya Rushwa ambavyo vinarudisha nyuma
maendeleo na kupindishwa kwa haki katika jamii.kuzingatia maadili ya
utendaji kazi ndani ya utumishi huu.
Waziri
Mkuchika alitoa kauli hiyo katka hotuba yake akiongea na wajumbe wa
kikao cha ushauri Mkoa wa Katavi (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano Idara ya Maji Wilayani Mpanda Mkoani Katavi mwishoni mwa
wiki.
Alisema
katika hatua ya makusudi ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na
kudhibiti utovu wa maadili ya watumishi wa umma,Serikali imeanzisha
Kamati za Uadilifu (Itegrity Committees) katika kila wizara, Idara na
Wakala zake zote.
Akifafanua
zaidi alieleza kuwa kamati hizo zilianzishwa pia katika mamlaka zote za
Serikali za Mitaa ,alitoa changamoto kwa Viongozi kuzitumia ipaswavyo
kamati hizo kwa kupokea taarifa za vitendo vya watumishi wasiokuwa
waadilifu na kuzifanyaia kazi ikiwa ni jitihada za kuongeza uadilifu
katika maeneo ya Kazi.
Kuhusu
Rushwa alisema kuwa inapotawala sehemu za Kazi husababisha madhara
mengi kwa jamii na pia misingi ya utawala Bora, madhara hayo yanaweza
kuhatarisha uhai na usalama wa Taifa,ikiwa ni pamoja na kutotimiza
utekelezaji wa majukumu ya serikali na kukwamisha utoaji wa haki na
husbabisha kuongezeka kwa maovu katika jamii.
Aidha
madhara mengine husababisha wananchi kukosa imani na serikali yao na
kujichukulia sheria mikononi.,athari nyingine ni kukosekana kwa huduma
muhimu za kijamii, kutolewa kwa huduma duni,kuwa na viongozi wasio
waadilifu na vilevile husababisha kupungua kwa pato la Taifa na hivyo
kupunguza uwezo wa serikali katika kuwahudumia wananchi.
Akasisitiza
kuwa kwa misingi hiyo Viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa kuhakikisha
wanakemia hali ya ummonyoko wa maadili na kurudisha maadili katika
misingi yake ya haki akawaomba wasaidiane na serikali kuratibu vipindi
vya dini mashuleni kwa
Akichangia
katika kikao hicho mmoja wa wadau Padri Peter Nguma wa Kanisa katoliki
alieleza kuwa vijana kukosa Elimu ya Vpindi Mashuleni inasaidia sana
kushusha maadili mashuleni hivyo aliomba serikali irudishe masomo ya
dini mashuleni.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi awali aliwahimiza watendaji wote
kujipanga katika kutekeleza Vipaumbele vilivyopo katika Mkoa ili kuleta
maendeleo katika mkoa.na kuwataka watumishi waumma katika mkoa huo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Katika
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa aliwahimiza watendaji wa Halmashauri zote
mkoani humo kuhakikisha makusanyo ya ndani yanapatikana kwa kuongeza
nguvu katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili Halmashauri ziweze
kujitegemea kwa sehemu kubwa katika bajeti yake kuliko kutegemea sehemu
kubwa ruzuku.
Aidha
akizungumzia kuhusu maeneo ya kuongeza mapato kwa upande wa Halmashauri
ya wilaya ya Nsimbo aliwahimiza kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwa
kushirikiana EPZ walioonesha nia ya kuwekeza katika eneo la maonesho ya
Nanenane.
No comments:
Post a Comment