MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Salu Geta(50) mkazi wa kijiji cha
Masawe mkoani Simiyu amekutwa akiwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia
mkanda wa Suruali katika kanisa la Anglikana lililopo kijiji cha Serengeti
wilayani Bunda mkoani Mara.
Kaimu
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mara Claud Kanyorota amethibitisha kutokea
kwa tukio baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na kwenda eneo la tukio abapo walimkuta mtu huyo akiwa amejinyonga.
Kanyorota
ameitaka jamii kuacha tabia ya kuchukua maamuzi ya kujinyonga na kama
kuna kuwa na shida ya yoyote ni vyema kuchukua maamuzi ya kutafuta
ushauri kuliko kujinyonga na kupoteza uhai.
Amesema
sio vyama kwa mwananchgi kuchukua maamuzi ya kujinyonga ata kama kuna
kitu kimemuumiza bali ni vyema kuchukua maamuzi ya kumuona mtu wa karibu
yake na kuomba ushauri juu ya kitu ambacho kinamsumbua
No comments:
Post a Comment