TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati
Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa ajili
ya kikao cha dharura, Februari 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Katika
kikao hicho, Kamati Kuu itajadili na kufanya uteuzi wa mwisho wa jina
la mgombea ubunge wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,
mkoani Iringa, unaotarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Kikao
hicho kitafanya uteuzi wa mwisho, baada ya mchakato wa ndani wa kumpata
mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CHADEMA, kuwa umepitia
hatua za awali, ambazo ni pamoja na watu wote wenye nia ya kugombea,
kuchukua fomu za uteuzi wa ndani tangu Februari 5-10, mwaka huu.
Kama
ilivyoelezwa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Februari 6, mwaka huu,
fomu hizo zilitolewa katika maeneo matatu, Ofisi za Makao Makuu ya
Chama, Dar es Salaam, Ofisi za Jimbo la Kalenga na kwenye tovuti ya
chama, ambayo ni; www.chadema.or.tz.
Jumla
ya watu 16 waliweza kuchukua fomu za kuwania uteuzi huo, ambapo hadi
siku ya mwisho, watu 13 waliweza kurejesha fomu zao na kupita kwenye
mchakato wa kura za maoni, zilizofanyika Februari 12, mwaka huu.
Imetolewa leo Februari 13, 2014, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
No comments:
Post a Comment