Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 14, 2014

UMRI WA MCAMEROON WALETA GUMZO BARANI ULAYA: ADAI ANA MIAKA 17 - SHIDA ZA KIMAISHA UTOTONI ZIMEMKOMAZA


Moja ya story kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka wiki hii inamhusus mchezaji mpya wa klabu ya Lazio Joseph Minala, ambaye watu wengi wamekuwa na mashaka na umri sahihi wa kiungo huyo wa Cameroon kwamaba ana miaka 17 au 40 na zaidi.

Kulikuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, akionekana kukasirishwa na kejeli na matusi ya mashabiki Joseph Minala aliamua kujibu mapigo kwa ujumbe wenye maneno makali kupitia akaunti yake ya Twitter kabla ya kuifunga, pia akaifunga ya Facebook na kuiweka ya instagram private.

Wakala wake Diego Tavano nae amezungumzia suala hili huku akimtetea mteja wake kwamba "shida za kimaisha" zimechangia muonekano wa kiutuzima wa mteja wake. Akiongea na Gazzetta dello Sport alisema: "Suala la Joseph Minala lipo wazi. Alikuwa amelelewa kwenye mazingira ya shida sana wakati wa udongo wake, hali iliyopelekea muonekano wake huu wa hivi sasa."
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Mmiliki wa klabu iliyomuuza kwenda Lazio, bwana Mauricio Perconti, nae alimtetea: "Siwezi kukataa kwamba anaonekana mtu zima sana, lakini vielelezo vyote vinaonyesha umri wake ni miaka 17."


TAZAMA PICHA ZA MINALA KISHA TOA MAONI YAKO. UNADHANI ANA MIAKA 17 KWELI?na shafih dauda
BgR 1SJCEAEbzPz Joseph Minalas agent says his 17 year old client who looks 40 appears older because of a difficult childhood
BgDmZIgIgAAbpp2 Joseph Minalas agent says his 17 year old client who looks 40 appears older because of a difficult childhood


No comments:

Post a Comment