Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 19, 2014

Akamatwa na kete 61 za cocaine JNIA Dar

Kamanda wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa

Mkazi wa Buguruni, Dar es Salaam (Jina linahifadhiwa) amedaiwa kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na kete 61 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Akizungumza jana, Kamanda wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema mtuhumiwa aliwasili JNIA akitokea Brazil akipitia Ethiopia akiwa amepanda ndege ya Shirika la Ethiopia.
Alisema Machi 17, mwaka huu saa 8:25 usiku, mtuhumiwa akiwa na hati ya kusafiria AB362172 ya Tanzania, alishukiwa na polisi kuwa amemeza dawa za kulevya.
Alisema baada ya kumtilia shaka walimhoji na kubaini kuwa amemeza dawa hizo ambapo alizitoa kwa awamu mbili ya kwanza akitoa kete 31 na baadaye 30.
“Aliposhuka kwenye uwanja wa ndege tulikuwa na wasiwasi naye na tulimchukua na kumhoji kwa zaidi ya saa moja baadaye alikubali kuwa amekula kete hizo ambazo alizitoa kwa njia ya haja kubwa,” alisema na kuongeza:
“Ninavyoongea na wewe mtuhumiwa bado anahojiwa na anaendelea kuzitoa dawa hizo,” alisema Kamanda Nzowa.
Kamanda Nzowa alisema upelelezi ukikamilika kesi yake itasikilizwa kwenye Mahakama Kuu kutokana thamani ya dawa aina ya cocaine kuwa kubwa.
“Kete moja ina gramu 17, gramu moja inauzwa Sh60,000 ambapo ipo tofauti na dawa aina ya heroine ambayo thamani yake ipo chini,” alisema Kamanda Nzowa.
 Chanzo;Mwananchi

No comments:

Post a Comment