Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 15, 2014

HIVI UNAJUA KUWA MWANAMKE HUPEVUKA KIAKILI MAPEMA KULIKO MWANAUME BASI SOMA UJUE UKWELI WAKE

Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana. Msichana akili yake huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba pindi wanapolea mtoto wa kike husogea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea mtoto wa kiume,” anasema Tuzie.
Imekuwa ni dhana ya muda mrefu miongoni mwa wanajamii katika Afrika  kuwa   msichana hawezi kuolewa na mwanamume waliyelingana umri kwa kuwa ni vigumu kuelewana na kuheshimiana. 
Dhana hiyo inajikita katika kuchambua tofauti ya ufahamu kati ya mwanamke na mwanamume wenye umri sawa. Mwanamke huwa na akili iliyokomaa zaidi kuliko mwanamume wa umri huo huo. Utafiti mpya umeipa uzito nadharia yao, baada ya kugundua kuwa ubongo wa msichana hukomaa haraka kuliko wa mvulana.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle wamasema hii inaweza kusaidia kuelezea sababu za wasichana wadogo kuonekana kukua kwa kasi zaidi, kuliko wenzao wa kiume wenye umri sawa.
Wanasayansi walitumia kipimo  maalumu kwa ajili ya kuchunguza ubongo kwa watu 121 waliokuwa na umri kuanzia miaka minne hadi 40. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba mchakato wa kubalehe huanza  kati  ya miaka 10 kwa msichana, huku mvulana huchukua muda mrefu kuanzia miaka 11 mpaka 20.
Dk.  Marcus Kaiser, ambaye nbi mtafiti, anasema: “Hii ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kujifunza ubongo kwa jumla.
 “Kwa kawaida hata katika utambuzi, imeonekana kwamba msichana ana uwezo wa kushika mambo mengi zaidi kuliko mvulana, ndiyo maana katika nchi za Afrika mtoto wa kike anapika, anajaribu kutekeleza majukumu ya nyumbani kama mama yake, bado shuleni atafanya vizuri, lakini si kwa mvulana. Akishazongwa na mambo mengi hupunguza morali shuleni.”
Dk. Kaiser anafafanua kuwa hatua za ukuaji wa mtoto wa kike ni za haraka ukilinganisha na wa kiume. Hii inatokana na mfumo wa kike. Binti hukua haraka kutokana na homoni zake mwilini na pia akishabalehe ndipo anakuwa na uelewa mpana kutokana na via vyake vya mwili kumruhusu kubeba ujauzito.”
Wataalamu nchini 
Tuzie Edwin, ambaye ni msemaji wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Kituo cha Huduma ya Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH), anasema mtoto wa kike huanza kupevuka kiakili ndani ya miezi mitatu baada ya kuzaliwa.
“Ukuaji wa ubongo wa mtoto wa kiume na wa kike ni tofauti sana. Akili ya Msichana huanza kukua kumzidi wa mvulana ndani ya miezi mitatu ya mwanzo tangu kuzaliwa. Katika uchunguzi wa wazazi watagundua kwamba wakati wanapomlea mtoto wa kike, huongea haraka zaidi kuliko wakati wa kulea mtoto wa kiume,” anasema Tuzie na kuongeza:
“Msichana hutambaa na kutembea haraka zaidi ukilinganisha na mvulana, hata katika kuongea. Pia huwa na uelewa mpana wa mazingira, anakuwa mwepesi kuanza kutumia choo mapema na ana kumbukumbu kwamba hivi sasa anahitaji kujisaidia na pia huanza kujitegemea ndani ya miaka miwili ikilinganisha na wa kiume,” anasema Edwin.
Anasema msichana huwa mwepesi katika kuwasiliana na pia huweza kuanza kushirikishwa katika baadhi ya mambo, kama kutumwa dukani mapema zaidi ukilinganisha na mvulana.
“Msichana pia anawahi kupevuka ukilinganisha na mvulana, lakini akishabalehe tu ubongo wake hukomaa haraka na hapo ndipo maumbile yake yanapoanza kujitengeneza mapema kwa ajili ya mwili kujitayarisha kubeba ujauzito wakati wowote. Hata hivyo akili yake hukua kwa nafasi kubwa kipindi hiki, ukilinganisha na mwanamume ambaye ni hadi miaka 10 baadaye,” anasema Edwin.
Mkurugenzi  wa Idara ya Sayansi katika Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Elifatio Towo anasema mtoto yeyote ana uwezo wa kukua kwa haraka zaidi, kutokana na namna mzazi anavyomlisha na haina tofauti na jinsi yake.
“Ikumbukwe kwamba mtoto yeyote anaweza kukua kwa haraka zaidi ikiwa mzazi atampa lishe bora na matunzo mazuri.
Kunyonyesha ndiyo sababu pekee inayowafanya watoto akili zao zikue kwa haraka zaidi. Lakini ikumbukwe kwamba watoto wa kike huwa na busara zaidi katika baadhi ya mambo na katika kufanya uamuzi ikilinganishwa na wa kiume,” anasema na kuongeza:
“Huyu anaweza kufikiria makubwa zaidi ya umri alionao, lakini mara nyingi inatokana na maumbile kwamba yeye  ni mwanamke hivyo kupevuka na anakuwa tayari kubeba ujauzito, mwili wake unajitengeneza wenyewe,” anasema Dk. Towo.
Wasemavyo wazazi
Maimuna Jitegemee, mama  mwenye watoto watatu, anasema “Binti yangu niliweza kumwachia nyumba akiwa na umri wa miaka 13 tu, niliweza kusafiri na kurudi. Hata hivyo hali imekuwa tofauti kwa mtoto wangu wa kiume, kwani licha ya kwamba dada yake yupo chuoni hivi sasa, siwezi kumwachia nyumba japokuwa ana umri wa miaka 15.”
 MWANANCHI

No comments:

Post a Comment