Moshi
Hussein ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi nyumbani kwa baba yake
mzazi huko katika kijiji cha Magiri wilaya ya Uyui mkoani Tabora,binti
huyu ana umri wa miaka 13 hajawahi kupelekwa Shule kwa maana ya kupata
haki kama wapatavyo watoto wengine,Moshi amekuwa akililia hilo kwa baba
yake mzazi bila mafanikio.Jambo baya zaidi kwa mujibu wa maelezo ya
Moshi baba yake anahitaji aolewe ili aweze kupata Ng'ombe licha ya kuwa
ana umri mdogo na hawezi kukabiliana na Changamoto za ndoa kulingana na
ulemavu alionao.
Moshi
kwakuwa hana uwezo wa kutembea umbali hata wa hatua kumi anawaomba
wasamalia wema kumsaidia mambo makubwa matatu,kwanza ikibidi kumuondoa
nyumbani kwao ili aepukane na ndoa ya lazima,Pili apelekwe shuleni
kwakuwa anaona kukaa kwa baba yake ni wazi kwamba atakuwa anatafuta
umasikini mwingine wa ziada ukiachana huo wa ulemavu wa viungo ambao
umekuwa kikwazo kikubwa hata cha kujihudumia masuala mengine ya kiutu wa
mwanamke.Kwa mujibu wa maelezo yake Moshi ana mshangaa baba yake kwa
uamuzi wa kutaka aolewe kwakuwa hata ndoa yenyewe haoni kama itakuwa na
maana kutokana na ulemavu alionao na pia haoni sababu ya kuwa mzigo kwa
mtu mwingine katika maisha yake.
Moshi
amekuwa akijikatia tamaa kulingana na ulemavu alionao,"Kama ningekuwa na
mama labda hata ningeweza kupelekwa shule na mimi ningekuwa msomi kama
wengine,lakini kwa hali hii ni bora hata ningekufa nimfuate mama yangu
huko aliko"
Via KapipiJHabari
No comments:
Post a Comment