Makamu mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania
Bara Bw Philip Mangula ameongoza
mamia ya wakazi wa mkoa
wa Iringa katika mazishi ya aliyekuwa
shekh mkuu wa waislam mkoa wa Iringa Alli Tagalile aliyefariki
asubuhi ya leo katika Hospital ya Rufaa ya mkoa
wa Iringa.
Mangula ambae katika mazishi hayo alimwakilisha
mwenyekiti wa CCM Taifa Raid
Dr Jakaya Kikwete alisema kuwa
Rais Dr Kikwete alipenda kushiriki mazishi hayo ila kutokana
namajukumu ameshindwa na kumwagiza yeye
kumwakilisha.
Hata hivyo alisema kuwa mwenyekiti wake Rais Dr
Kikwete hakuweza kupata nafasi
ila amesikitishwa sana na kifo
cha Shekh Tagalile na kuwa Shekh huyo
atakumbukwa kwa mambo mengi ambayo amepata kuyafanya
enzi za uhai wake.
Mangula alisema kwa mambo makubwa aliyoyafanya marehemu
Tagalile enzi za uhai wake iwapo yangeandikwa na kuwekwa katika vitabu vya kumbu bumbu ni zaidi ya
kitabu kimoja ambacho kingeelezea mambo yake.
Mwakilishi wa mufti wa baraza kuu la Waislam Tanzania
katika mazishi hayo Shekh Omary
Nzowa alisema kuwa mufti mkuu wa Waislam nchini alitegemea kufika
katika mazishi hayo ila kutokana
na kuwa nje ya nchi hakuweza kufika
japo ametuma salam zake kwa waislam mkoa wa Iringa .
Alisema kuwa
Shekh Tagalile enzi za uhai
wake alikuwa ni mwakilishi wa Mufti katika mkoa wa Iringa hivyo kifo chake
kimeacha pengo kubwa katika mkoa
wa Iringa na nje ya mkoa.
Hata hivyo alisema kuwa baraza la waislam mkoa wa Iringa linawapongeza
wakazi wote wa mkoa wa Iringa pamoja na viongozi mbali mbali wa dini hiyo ya Kiislam na dini nyingine na
wale wa vyama
vya siasa ambao wamepata kushiriki akiwemo Bw Mangula.
Shekh Tagalile atakumbukwa kwa mchango wake
mkubwa ambao aliutoa enzi za uhai wake ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali
katika kuwahamasisha watanzania kujitokeza katika sense ya watu na makazi mwaka 2012.
Kwa upande wake
mkuu wa mkoa wa Iringa Dr
Christine Ishengoma akielezea kifo hicho alisema
kimeacha pengo kubwa katika mkoa na kuwataka viongozi na
wananchi wa mkoa wa Iringa
kuendelea kumuenzi kwa mema yote
aliyotenda .PICHA NA HABARI NA FRANSIS GODWIN
|
No comments:
Post a Comment