Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 11, 2014

MWALIMU WA MAREHEMU DR.WILLIAM MGIMWA AMUOMBEA KURA MJUKUU WAKE GODFREY MGIMWA KALENGA

1Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara akimkumbatia mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Mapinduzi Bw. Godfrey Mgimwa kwenye eneo la Tosamaganga kata ya Kalenga mahali ambapo mkutano wa hadhara wa kampeni umefanyika  ikiwa ni mfurulizo wa mikutano hiyo iliyofanyika katika vitongoji na vijiji vya kata ya Kalenga. Uchaguzi wa jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16 jumapili ijayo ambapo Mzee Philip Mangula amewaomba wananchi wa Kalenga kumchagua Godfrey Mgimwa wa CCM kwa kura nyingi za ndiyo.(PICHA NA KIKOZIKAZI CHA FULLSHANGWE-KALENGA) 1aSister Paula Msambwa miaka 75 ambaye pia ni muuguzi katika hospitali teule ya Tosamaganga na mwalimu wa Marehemu Dr.William Mgimwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo akitoa ushuhuda wake na kufurahia kumuona mjukuu wake Godfrey Mgimwa akigombea ubunge katika jimbo la Kalenga Sister Paula amekiri na kusema Marehemu Dr.William Mgimwa alipenda sana somo la hesabu na alikuwa ni mwanafunzi mwenye kipaji na nidhamu 2aSister Paula Msambwa miaka 75 ambaye pia ni muuguzi katika hospitali teule ya Tosamaganga akimuonyesha mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa na kusema nimefurahi sana kuona mjukuu wangu akigombea ubunge.
3Mwenyekiti wa CCM Iringa vijijini Bi. Delfina Mtavilalu kushoto na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi. Jesca Msambatavangu wakipiga magoti kumuombe kura za ndiyo Bw. Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Tosamaganga. 4Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa akipokelewa kwa nderema na vifijo mara baada ya kuwasili katika mji wa Kalenga mahali ambapo amefanya mkutano wa hadhara  na kuomba kura za ndiyo kwa wananchi. 4aMgombea ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juujuu mara baada ya kuwasili Kalenga  tayari kwa kufanya mkutano wa kampeni. 5Wananchi wakimpokea mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Bw. Godfrey Mgimwa kwa picha zake mara baada ya kuwasili katika kitongoji cha Ipamba kata ya Kalenga 8Msanii Dokii akiimba pamoja na wananchi katika kitongoji cha Ipamba kata ya Kalenga 9Akina mama wakionyesha picha za Bw. Godfrey Mgimwa kama ishara ya kumkubali. 10Mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM Bw. Godfrey Mgimwa akisalimiana na Masister mbalimbali wa parokia ya Tosamaganga 11Wananchi wakinyanyua mikono yao juu kama ishara ya kumkubali mgombea huyo wa CCM. 12Chifu Abdull Mkwawa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Kalenga 14Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula akiwaelekeza wananchi jinsi ya kupiga kura siku ya jumapili machi 16 ambapo amewaomba wanakalenga kwa ujumla kumchagua Bw. Godfrey Mgimwa wa CCM

No comments:

Post a Comment