Mgeni rasmi Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Edward Rutakangwa (katikati) akiwasili kufungua rasmi mafunzo ya
siku nne juu ya sheria za kimataifa za kazi kwa majaji na wasajili wa
mahakama nchini yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani mjini Bagamoyo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi duniani kwenye nchi
nne Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, Alexio Musindo.
Na Damas Makangale, Bagamoyo, MOblog Tanzania
JAJI wa Mahakama ya Rufani,
Tanzania, Edward Rutakangwa amesema bado kuna upungufu mkubwa wa majaji
katika mahakama za Tanzania kiasi cha kusababisha mrundikano wa kesi
katika mahakama hapa nchini. MOblog inaripoti.
Akifungua rasmi mafunzo ya siku
nne kwa majaji, wasajili na wasajili wasaidizi wa Mahakama ya Kazi, Jaji
Rutakangwa amesema kwamba pamoja na Mheshimiwa wa Rais kuteua majaji
bado kuna upungufu mkubwa wa majaji nchini.
“Tatizo la majaji kuwa wachache ni
la muda mrefu pamoja na juhudi za Mheshimiwa rais kupunguza ukubwa wa
tatizo kwa minajili ya kuleta ufanisi katika idara ya mahakama,” amesema
Jaji Rutakangwa. Amesema mafunzo hayo ya siku nne yataleta matokeo
mazuri kwa majaji na wasajili wa mahakama katika kuleta haki kwa
wafanyakazi na kufanya kazi kwa viwango vya kimataifa vya kazi duniani.
Meza kuu ikipitia makabrasha yao
kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mafunzo hayo. Jaji Rutakangwa
alilisisitiza kwamba kuna umuhimu wa majaji kujua haki na sheria za kazi
kwa hiyo mafunzo hayo yatatoa fursa kwao kuelewa sheria za kazi ili
kuwawezesha kutoa hukumu kwa kuzingatia sheria na haki za wafanyakazi
nchini.
Amesema kuna umuhimu wa majaji na
wasajili wa mahakama kuelewa kwa kina sheria za kimataifa za kazi na
jinsi ya kuzitumia katika mahakama za ndani ya nchini. Kwa upande,
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kazi Duniani, Kenya, Tanzania,
Rwanda na Uganda, Alexio Musindo amesema Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa
walifanya mabadiliko kadhaa ya kijamii na kiuchumi.
Mmoja wa wawezeshaji kutoka Ghana akijitambulisha kwa washiriki wa mafunzi hayo.
Amesema moja ya mipango ya
serikali hizo mbili ni kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya soko huria
pamoja na kuweka vyombo vya kudhibiti soko hilo kama vile Mahakama ya
kazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
“Shirika la kazi duniani
litaendelea kufanya kazi kwa karibu na mahakama ya kazi pamoja na Tume
Usuluhishi katika kuleta ufanisi katika sekta ya kazi kwa kujali maslahi
ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi duniani,” amesema Musindo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani, Edward
Rutakangwa akifungua rasmi mafunzo ya siku nne juu ya sheria za
kimataifa za kazi kwa majaji na wasajili wa mahakama nchini
yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani mjini Bagamoyo.
Musindo amesema katika mafunzo
hayo yatatoa fursa kwa majaji na wasajili wa Mahakama kujifunza sheria
za kimataifa za kazi na utatuzi wa migogoro katika sehemu za kazi.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mgaya amesema kwa kuwa sheria ya
kazi ni mpya ya mwaka 2004 bado kuna majaji na wasajili wa mahakama
haifahamu vya kutosha ili kukidhi haya ya jamii.
Amesema mafunzo hayo ya siku nne
ni fursa pekee kwa majaji na wasajili wa mahakama kujifunza sheria za
kimataifa za kazi ili kuleta tija katika maamuzi yao mbalimbali.
Baadhi ya majaji na wasajili wa
mahakama nchini wanaohudhuria mafunzo ya siku nne juu ya sheria za
kimataifa za kazi yalioandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mjini
Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa
la kazi duniani (ILO) kwenye nchi nne Tanzania, Kenya, Rwanda na
Uganda, Alexio Musindo akizungumza na washiriki kwenye mafunzo hayo
mjini Bagamoyo.
Jaji Regina Rweyemamu kutoka
Mahakama ya kazi, akizungumza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
kama majaji katika mahakama za kazi nchini.
Baadhi ya majaji na wasajili wa
mahakama nchini wakifuatilia yanayojiri kwenye ufunguzi wa mafunzo ya
siku nne yaliyoandaliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) yanayoendelea
mjini Bagamoyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw. Nicholas Mgaya akizungumza na washiriki
wa mafunzo hayo ya siku nne kuhusu changamoto katika mahakama za kazi,
upungufu wa majaji na vitendea kazi kama moja ya vitu vinavyochangia
mrundikano wa kesi katika mahakama hapa nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri
(ATE) Wakili, Cornelius Kariwa akitoa hotuba yake kwa niba ya chama cha
waajiri nchini umuhimu wa kufahamu sheria za kimataifa za kazi duniani.
Baadhi ya wasijili wa Mahakama ya kazi wakiwa kwenye mafunzo ya siku nne yanayoendelea mjini Bagamoyo.
Mgeni rasmi Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Edward Rutakangwa (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi
wa Shirika la Kimataifa la kazi duniani (ILO) kwenye nchi nne Tanzania,
Kenya, Rwanda na Uganda, Bw. Alexio Musindo wakati wakielekea kupiga
picha ya pamoja. Kulia ni Afisa Mipango mwandamizi wa shirika la kazi
duniani (ILO) Anthony Rutabanzibwa.
Mgeni Rasmi Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Edward Rutakangwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
mafunzo hayo ya siku nne yanayoendelea mjini Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment