.Waziri alimburuzwa mahakamani kwa kosa la kukiuka sheria za ajira
. Ashinda kesi kiaina baada ya Mahakama ksuema hakuna ushahidi wa kutosha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NAIBU
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga
ambaye aliingia katika kashfa nzito ya kuvunja sheria za kazi nchini kwa
kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake Bunge kwa miaka kumi
bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki mbili tu (200,000)
kama mafao ameshinda kesi hiyo. Imeripotiwa
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Wakili
wa Bi Itika Kasambala (31) Bw, Nyaisa Godwin amesema kwamba mahakama
iliona hakuna ushahidi wa maandishi kati ya mwajiri na mwajiriwa.
“unajua
sikia kwa sababu waziri mwenye dhamana ya kazi kumplekea mahakama ya
kazi ni vigumu sana kushinda kesi kutokana na mazingira ya utendaji kazi
katika sehemu nyingi za serikali na mahakama,”
“lakini
kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha yaani mkataba wa maandishi kati ya
waziri na Bi kasambala na huo ndio ugumu wenyewe,” amesema Wakili Nyaisa
Amesema
kuwa kwa sasa hawezi kuongea zaidi kwa sababu hilo ni jukumu la
mlalamikaji kuamua hatua zaidi za kufuata baada ya maamuzi ya mahakama
kutolewa.
Awali
akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakili, Nyaisa amesema kuwa kesi
imefunguliwa mahakama ya kazi wiki iliyopita siku ya Jumanne, Tume ya
Usuluhishi na Upatanishi kesi namba CMA/DSM/ILA/R.711/13.
Wakili
Nyaisa alisisitiza kwamba Naibu Waziri aliiambia mahakama kwamba Dada
Kasambala alikuja kufanya kazi kwake kama mwanafunzi wa chuo kwenye
mazoezi lakini alishidwa kuithibitishia mahakama kwa ushawishi wa barua
ya (field to chuoni).
“tulishagazwa
na majibu ya waziri kwamba dada huyo alikuwa field, na nilimuuliza
field ya miaka kumi? Alishidwa kutoa jibu mbele ya mpatanishi
(Arbitrator),” amesema Nyaisa.
Nyaisa
aliendelea kusema kutokana na matatizo ya kuachishwa kazi ghafla bila
taratibu dada huyo amepata maradhi ya presha, vidondo vya tumbo na
maradhi mengine baada ya kufanya kazi kwa Mhe Mbunge kwa miaka kumi bila
matibabu wala kulipiwa mifuko ya hifadhi za jamii.
Awali
Bi kasambala alisema alianza kazi kwa Mbunge huyo wa Segerea na Naibu
Waziri wa kazi Dkt Mahanga, mwaka 2003 kama PS (Personal Secretary) kwa
makubaliano ya kumpa mshahara wa shilingi 120,000 kwa mwezi lakini
alianza kumlipa shilingi 50,000 tu.
“aliniambia
kwamba nianze kazi kwanza baadaye atanipa mkataba wa ajira na kunilipa
mafao ya hifadhi ya jamii na matibabu lakini baada ya miaka kumi
ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi basi sikuhitaji tena,” Kasambala
amesema.
Amesema
kwamba Mbunge huyo alimtumia sms akiwa kwenye vikao vya bunge mjini
dodoma mwaka jana mwezi wa sita akimjulisha kwamba ajira yake imeshafika
kikomo kwa sababu hana uwezo tena wa kumlipa mshahara na mahitaji
mengine ya kiofisi.
Kasambala
aliendelea kusema kwamba mara ya kwanza wakati anaanza kazi mwezi wa
tano mwaka 2003 baada ya msaidizi wa ofisi ya mbunge Mahanga kuacha kazi
na ndipo alipotafutwa yeye na walikwenda kuelewana kwa malipo ya
120,000 kwa mwezi.
Alisisitiza
kwamba mara baada ya kuanza kazi kwa ofisi ya mbunge alikuwa analipa
pesa kupitia mkononi na baadaye tigo pesa na baada ya muda akawa
anachukua pesa yake ya mshahara toka katika manisapaa ya Ilala kama
posho ya mhe mahanga kama diwani kila mwezi.
Dada
huyo kwa mshangao baada ya mahojiano ya muda mrefu alikiri kwamba mhe
mahanga alikuwa na nia ya dhati kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na
kumtaka aende Dodoma lakini alikataa kufanya mashati hayo.
“mwaka
juzi baada ya kuonyesha nia ya kunitaka kimapenzi alinipigia simu
akitaka niende Dodoma bungeni kwa mazungumzo zaidi kama msaidizi wake
lakini nilikataa,’ aliongeza Kasambala
Amesema
tangu aanze kazi kwa Mhe Mahanga hakuwa anatoa huduma zozote kama
matibabu au fedha kwa ajili ya sikukuu ilikuwa ni mshahara tu wa 120,000
kwa mwezi lakini kila akimfuata ili waandikishiane mkataba alikuwa
akizungumsha bila sababu za msingi.
Bi
Kasambala aliongeza kuwa amefanya kazi Mhe Mahanga tangu akiwa mbunge wa
Ukonga na baadaye Segerea lakini ameshidwa kuheshimu sheria za ajira na
taratibu za kazi wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana ya ajira
kwa watanzania.
Amesema
mwaka jana tarehe 14/09/2013 alimtumia kwa Tigopesa kiasi cha shilingi
za Tanzania 200,000 kama mafao yake baada ya kufanya kazi kwa takribani
miaka 10 kama Msaidizi wake wa Ofisi ya Mbunge.
Amesema
kwamba aliamua kwenda Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahoteli,
Majumbani na Kazi Nyingine (CHODAWU) kwa msaada wa ksiheria ba baada ya
kukutanishwa bado Mhe Mahanga akawa mgumu kukubaliana kiungwana mpaka
ikawalazimu kwenda mahakani Tume ya Usuluhishi na Upatanishi.
Kwa
sasa baada ya hukumu kutoka tarehe 13/02/2014 katika mahakama ya kazi
(Tume ya Usuluhisho na Upatanishi ameamua kupeleka shauri lake kwenye
Shirika la Kazi Duniani (ILO) jijini Dar es Salaam ili haki itendeke.
Kwa
mujibu wa sheria kazi na mahusiano kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu
cha 3 cha sheria ya Taasisi za kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka
sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na sehemu ndogo A kwa kushidwa
kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara ya kwanza kama
sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.
Katika
kifungu hicho cha 14 ibara ya kwanza kinasema mkataba utakuwa wa
kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi maalumu na mkataba unatakiwa
kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu Waziri hakufanya.
Ibara
ya 15 kifungu cha.-(1) kinasema kwa kuzingatia masharti ya kifungu
kidogo cha (2) cha kifungu cha 19, mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi,
wakati mfanyakazi anapoanza kazi, taarifa zifuatazo kwa maandishi, jina,
umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi; mahali alipoajiriwa;
kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo na muda wa mkataba; kituo cha kazi;
masaa ya kazi; ujira na njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao
mengine
No comments:
Post a Comment