Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 11, 2014

SHINA LA CCM MARYLAND LAFUNGULIWA, MRISHO MZESE MWENYEKITI, MARCO MBULLU KATIBU

Mwenyekiti wa shina la CCM Maryland, Mrisho Mzese (tatu toka kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti CCM DMV George Sebo (pili toka kushoto) kwenye ufunguzi wa shina hilo uliofanywa na mwenyekiti huyo wa tawi CCM DMV siku ya Jumapili March 9, 2014 Germantown, Maryland. Picha na Vijimambo Blog
 Mwenyekiti wa shina CCM Maryland, Mrisho Mzese akiongea na kumkaribisha mwenyekiti wa CCM DMV George Sebo huku Mama Kimolo akifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti CCM DMV George Sebo akitoa shukurani zake kwa mwenyekiti wa shina Mrisho Mzese na kuwapongeza wanachana na wajumbe wa shina hilo akiwemo Katibu wa shina Marco Mbullu (hayupo pichani) kwa maamuzi ya ufunguzi wa shina hilo la Maryland uliofanyika siku ya Jumapili March 9, 2014, Germantown, Maryland.
Juu na chini ni Mwenyekiti wa CCM DMV akikabidhi bendera ya CCM kwa mwenyekiti na katibu wa tawi, wapili toka kulia ni mwenyekiti wa UWT CCM DMV Aunty Grace Mgaza Sebo.
Mwenyekiti wa CCM DMV, George Sebo akimsikiliza mwenyekiti wa shina CCM Maryland baada ya kumkabidhi kitabu cha ilani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa Shina CCM Maryland akimkabidhi kadi ya uanachama mmoja ya wajumbe washina hilo lililofunguliwa siku ya Jumampili March 9, 2014 Germantown, Maryland.
Viongozi wa CCM DMV katika picha ya pamoja na Viongozi wa shina CCM Maryland wakiwemo wajumbe na wanachama wao.

No comments:

Post a Comment