Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi Renatha Mzinga
Waya zilizokamatwa kwa mtuhumiwa Abdul Mahamud ambazo zimeyeyushwa zinasadikiwa kuwa za kampuni ya simu(TTCL)
..Baadhi ya madawa waliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Salum Shaban Mapande
Na Abdulaziz Video, Lindi
Watu
watatu wanashikiliwa na Polisi Mkoani Lindi kwa tuhuma za kukutwa na
madawa ya kulevya aina ya heroin pamoja na Miundo mbinu ya Kampuni ya
simu kinyume na Sheria.
Kamanda
wa Polisi
Mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi Renatha Mzinga amesema leo kuwa kwa
ushirikiano mkubwa waliopewa na wanajamii wamefanikiwa kumkamata Bw
Salum Shaban Mapande(32)Mkazi wa Dar es sallam akiwa na madawa ya
kulevya kete 42 kubwa na ndogo 104 zenye uzito wa Gram 58 na pesa
taslim tsh 2,827,500 zinazosadikika kuwa za mauzo ya madawa hayo
Watumiwa wengine waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha
Utalii mjini Lindi, Masudi Mohamed(19) aliekutwa na kete 35 za bhangi
huku Abdul Mahamud na Halfan Salum waliokutwa na nyaya za kampuni ya
simu TTCL Zenye Uzito wa kg 5.
Kamanda Mzinga alisema mkoa wa
Lindi umeanza kampeni kubwa ya kupambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo
kupambana na wimbi la uingizaji na uuzaji wa madawa ya kulevya
ambalo kwa sasa kuna ongezeko kubwa la utumiaji na uuzaji wa madawa
hayo ikiwemo pombe haramu ya gongo.
Aidha Kamanda Mzinga ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujidhatiti
na kufichua wahalifu wakiwemo wauza madawa ya kulevya ambapo Jeshi
lake litatoa ushirikiano na usiri kwa watakaotoa taarifa zinazoashiria
Uvunjifu wa Amani ikiwemo za Usalama barabarani
No comments:
Post a Comment