skip to main |
skip to sidebar
TAZAMA PICHA:: DEREVA WA MWIGULU NCHEMBA AKIWA HOSPITALINI BAADA YA KIPIGO NA WATU WANAODAIWA KUWA WAFUASI WA CHADEMA
DEREVA
wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Mohamed Kunambi,
ameshambuliwa na kujeruhiwa na watu wanaodhaniwakuwa wafuasi wa chama
cha CHADEMA.
Tukio hilo liletokea usiku wa kumkia leo eneo la Ifunda jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini mkoa wa Iringa.
Mbali na dereva huyo diwani wa kata ya Ifunda, Eliya Mngwila, naye amejeruhiwa na watu hao waliposhambulia gari alilopanda.
Hayo
yalielezwa jana na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, wakati
alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mchakato wa
kampeni.
Mtenga alisema tukio hilo lilitokea eneo Ifunda ambapo
vijana wa CHADEMA waliokuwa kwenye gari lenye namba za usajili T 156 CDA
iliyokuwa na nembo ya M4C inayotumiwa na chama hicho.
Alisema
vijana hao wakiwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapangawalimkuta dereva
huyo pamoja na viongozi wengine wa CCM akiwemo diwani huyo na kuanza
kuwashambulia.
Alisema baada ya tukio hilo waliojeruhiwa
walipelekwa Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Iringa abako waliandika
maelezo na kupewa kibali cha kwenda hospitali (PF3).
"Walishambulia
magari yetu kwa kuyavunja vioo hivi sasa yako polisi, tunauhakika
waliofanya hivi ni wafuasi wa CHADEMA na hayo ni maelekezo kutoka kwa
viongozi wa juu wa chama hicho," alisema.
Kwa mujibu wa Mtenga, gari la CCM lililoshambuliwa ni lenye namba za usajili T 139 CKS ambalo pia liko Polisi.
Wakati
huo huo, CCM imesema CHADEMA imeingiza mkoani humo vijana 120 kwa ajili
ya kufanya vurugu ili kuvuruga mchakato wa uchaguzi huo.
Mtenga,
alisema taarifa za uhakika walizonazo, zinasema vijana hao wameingia
mkoani humo juzi na watasambazwa kwenye kata mbalimbali za jimbo hilo.
"Hivi
sasa vijana hao wako Iringa mjini wakijiandaa kutekeleza malengo yao
ambapo miongoni mwake ni haya yanayotokea sasa," alisema.
Mtenga
alikionya chama hicho na kusema kisithubutu kufanya vurugu hizo kwa
lengo la kumwaga damu kwa wananchi wasio na hatia kwani hakitavumiliwa.
"Kazi ya CCM ni kulinda amani, hivyo hatutakuwa tayari kuona damu ya mkazi yeyote wa Kalenga inamwagika," alisema.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu madai ya kutekwa Paroko wa Kanisa la Orthodox, Parokia
ya Mtakatifu Basil Mkuu , Costantino Mbilinyi, Mtenga alisema ni za
uongo.
Akifafanua kuhusu tukio hilo alisema CCM ina watu wenye akili timamu ambao hawawezi kufanya tukio hilo.
Kwa mujibu wa Mtenga, siku ya tukio Paroko huyo aliongozana na vijana saba wa CHADEMA kutoka Arusha kwa ajili ya kufanya vurugu.
Alisema
gari alilokuwemo paroko huyo lilikutwa na silaha za jadi yakiwemo
mapanga ambazo zinadhaniwa zilikuwa maalumu kwa ajili ya kufanyia
uhalifu.
"Mwaka 2010 paroko huyo alikuwa mpambe wa Grace Tendega
wakati huo akiwa cha cha Jahazi Asilia ambaye kwa sasa ndiye mgombea
ubunge kupitia chama cha CHADEMA," alisema.
No comments:
Post a Comment