Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 19, 2014

TIMU YA WAKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO KUTOKA TUME YA MIPANGO WATEMBELEA BONDE LA MAGADI SODA LA ENGARUKA NA ZIWA NATRON

 Moja ya Shimo la magadi soda katika Bonde la Engaruka.
  Picha inayoonesha moja ya mashimo yaliyochorongwa katika Bonde la Engaruka Wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha kuthibitisha uwepo wa hazina kubwa ya magadi soda. Hii ilidhihirishwa mbele ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango aliyeongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka katika ofisi yake (hawapo pichani).


 Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto) akionja maji ya magadi soda yaliyotoka katika moja ya shimo lilichorongwa katika bonde la Engaruka alipoongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango. Anayewamiminia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bw. Gideon Nasari.
  Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakijaziwa maji ya magadi soda katika chupa za maji ya kunywa walipotembelea bonde la Engaruka ambako kuna hazina kubwa ya magadi soda. 
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akitazama (admires) kipande cha magadi soda katika eneo la Ziwa Natron Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha alipoongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka katika ofisi yake. Pamoja naye ni watoto wa kimasai waliokuwa wakiuza vipande hivyo vya magadi soda.

No comments:

Post a Comment