skip to main |
skip to sidebar
UELEWA MDOGO WA WANANCHI JUU YA UENDELEZAJI WA MIRADI INAYOANZISHWA UMEPELEKEA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA MAJI NA MAENDELEO MAMADO KUCHELEWA KUTEKELEZA MIRADI YAKE.
Akizungumza na Dodoma FM Meneja Mipango wa Shirika la MAMADO Bwana
Agustino Rukeha amesema pamoja na shirika hilo kutoa Elimu ya
uendelezaji wa miundombinu bado jamii haijajenga dhana ya kujitolea
kuchangia kuendeleza miradi inayoanzishwa na mashirika mbalimbali.
Aidha Bwana Rukeha amesema pamoja na shirika hilo kufanya kazi kwa
kufuata sera ya nchi ya wananchi kuchangia lakini bado jamii imekuwa
haina uelewa
wa kutosha katika suala la kuchangia.
Nae Kaimu Meneja Mipango wa shirika hilo Bwana Ernest Mella amesema
miradi mingi imekuwa ikichelewa kutokana na ushiriki mdogo wa jamii
kwani
wananchi wamekuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya uendelezaji wa miradi
No comments:
Post a Comment