Stori: Makongoro Oging’ na Harun Sanchawa
MAJONZI,
huzuni na masikitiko vimeikumba familia ya Lwena kufuatia mtoto wao
mpendwa Dorryce Lwena (27) kufariki dunia kwa kupigwa risasi mkono wa
kushoto na ubavu wa kushoto na watu wasiojulikana, Uwazi lilifuatilia.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwanzoni mwa mwezi huu, saa tatu
usiku, Uwanja wa Edosi, Kitunda, Ilala hatua chache kutoka nyumbani kwa
marehemu huyo.
Siku ya tukio, Dorryce ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu
Singida (DSA), alikuwa akitoka Kariakoo kununua vifaa vya kwenda navyo
chuo siku mbili mbele lakini kifo kilimkuta akiwa anakaribia kufika
nyumbani.
Kama ilivyo ada, baada ya kujulishwa tukio hilo la kikatili,
waandishi wa Uwazi walifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na baba
wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye baada ya baba mzazi
kutengana na mama yake.
Baba huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga alikuwa na haya ya kusema:
“Ilikuwa
Jumamosi, Machi Mosi, mwaka huu, saa tatu usiku nikiwa karibu na
kwangu, mke wangu (mama wa marehemu) alinipigia simu akaniambia kuna
risasi zimepigwa karibu na nyumba yetu, nikamwambia haraka sana wafunge
milango na mtu asitoke nje hadi itakapojulikana kuwa risasi hizo
zilikuwa za nini.
“Muda mfupi baada ya kuongea na mke wangu, dada wa Dorryce alinipigia
simu akiniambia nirudi nyumbani haraka kwani Dorryce amepigwa risasi na
amefariki dunia.
“Nina gari, niliingia ndani yake haraka tayari kwa safari ya kurejea
nyumbani. Nikiwa nakaribia nyumbani niliona kundi la watu, nilisogelea
eneo hilo na kukuta mwili wa Dorryce umelala katika dimbwi la damu.
“Nilikuta
familia yangu, akiwemo mama wa marehemu wakilia kwa uchungu. Iinibidi
nikatoe taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kitunda, nao walinishauri niende
Kituo cha Polisi Stakishari.
“Polisi walifika eneo la tukio na kufanya michoro kisha wakauchukua mwili hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Mke
wangu ana hali mbaya sana jamani. Tangu tukio hilo amekuwa akizimia
mara kwa mara, presha inapanda na kushuka. Naombeni msimhoji,” alisema
kwa masikitiko makubwa baba huyo.
Alisema mpaka siku hiyo familia ilikuwa haijui chanzo cha mauaji hayo.
Akasema: “Ninachokumbuka mimi siku hiyo mke wangu alimkataza marehemu
asiende Kariakoo lakini alikataa, akasema kwa vile Jumapili atakwenda
kanisani na Jumatatu ndiyo safari ya kurudi chuo, afadhali aende siku
hiyo.”
“Ila wakati marehemu yupo chuoni alizaa na mwanaume mmoja ambaye
tulimtaka amhudumie mtoto kwa vile mama yake bado anasoma lakini
alikataa, hivyo marehemu aliamua kumchukua mtoto na kumpa. Hadi hapo
tukawa hatuna uhusiano naye mzuri,” alisema mzee huyo.
Waandishi wetu walifanya mahojiano na majirani kutaka kusikia kama
wanajua lolote juu ya tukio hilo ambapo baadhi yao walisema mauaji hayo
hayajawahi kutokea eneo hilo na kudai kwamba marehemu ndiye anayejua
sababu ya kupigwa risasi.
“Marehemu baada ya kupigwa risasi ya kwanza alilia kwa uchungu na kupiga kelele kuomba msaada. Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza.
“Aliongezwa risasi ya pili sauti yake haikutokea tena, wale watu
walitimka na pikipiki ndipo wananchi tukajitokeza, nahisi ni mapenzi,”
alisema mwanamke mmoja anayefanya biashara karibu na eneo la tukio.
Baba mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Julius Jacob Lwena anayeishi Tabata Tenge, Dar yeye alikuwa na haya ya kusema:
“Kifo cha Dorryce kimeniuma sana, ila napenda kusema kwamba maisha yake kwa undani siyajui sana kwa sababu nilikuwa mbali naye.
“Mara ya kwanza marehemu alipomaliza elimu ya sekondari alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi, alirudishwa kutokana na ujauzito.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka Chuo cha Utumishi Singida, bahati
mbaya akapata mimba ya mwanaume mwingine, ikabidi arudi nyumbani.
“Baada ya kujifungua tulimpeleka chuo cha uhasibu Singida na mauti yamempata alipokuja likizo,” alisema mzee huyo.
Marehemu alizikwa Machi 4, mwaka huu katika Makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.CHANZO GPL
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAKAGUA UTEKELEZAJI
WA AFUA ZA UKIMWI NJOMBE
-
NA.MWANDISHI WETU
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, imetembelea miradi
mbalimbali mkoani Njombe leo tarehe 09 Januari, 2025.
Ka...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment