Aidha treni inayofanya safari zake kwenda Zambia na mikoa mingine zinatarajiwa kuanza kesho.
Baadhi
ya abiria waliokuwepo katika kituo cha makao makuu Dar es Salaam kwenda
Mwakanga walimwambia mwandishi kuwa wamefurahishwa na kuanza kwa safari
hizo.
Aidha watu waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kukuta
tiketi za kwenda mkoani walisema wameambiwa safari zote zitaanza Kesho.
“Kikubwa
tumefurahishwa na mgomo kuisha na safari kurejea kama kawaida,
tulishindwa kusafiri ila sasa hata kama ni Ijumaa hatuna budi kusubiri,”
alisema Juma Abdalah.
Naye Esta Danford alisema alihitaji kwenda kumuona mama yake ambae ni mgonjwa Zambia na alishindwa kutokana na mgomo huu.
“Mama
yangu ni mgonjwa sana kutokana na mgomo nilishindwa ila nashukuru kuona
safari zimerejea naamini sasa nitakwenda kumuona mama,” alisema
Danford.
Wafanyakazi hao ambao juzi walitangaza kusitisha mgomo huo ambao ulianza Mei 12 mwaka huu, baada ya mahakama kuubatilisha.
Ambapo wafanyakazi hao walikuwa wakigoma kudai kulipwa mishahara yao ambayo walikuwa wakiidai serikali.
Mgomo wa wafanyakazi ambao serikali imedai kupata hasara ya Sh bilioni 2.65.
No comments:
Post a Comment