Na Baraka Mbolembole
Timu ya soka ya Taifa ya Australia, maarufu kama '
Soccerrose' ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika
mchezo mmoja duniani. Australia waliichapa, American Samoa magoli 31-0, April 11, 2001 katika mchezo wa
kimataifa unaotambuli wa na FIFA...Soccerrose, walitua nchini, Brazil siku ya
jana tayari kwa michuano ya kombe la dunia inayotaraji kuanza kutimua vumbi,
juni 12. Australia ipo katika kundi la pili sambamba na mabingwa watetezi,
Hispania, makamu bingwa wa fainali zilizopita, Uholanzi, na Chile.
Kikosi cha kocha, Ange Postecoglou kimeshawahi kucheza
michuano hiyo mara tatu na mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya 16 bora,
mwaka 2006... Kwa mara ya kwanza, Australia, ilifuzu kwa fainali za mwaka 1974
zilizofanyika nchini Ujerumani na kuondoka patupu. Walipata suluhu-tasa dhidi
ya Chile, kisha wakapoteza kwa waliokuwa wenyeji wa michuano, Ujerumani
Mashariki, na Ujerumani Magharibi na kuondoshwa mashindanoni pasipo kufunga
goli lotote. Ikiwategemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama Tim Cahiil, na
nahodha wa kikosi hicho, Michael Jadinak ambaye anakipiga katika kikosi cha
Crystal Palece ya England ,kikosi hicho kimekuwa timu ya kwanza kuwasili,
Brazil.
Timu hiyo haina rekodi ya kutisha katika michuano ila katika
fainali mbili za mwisho wameonekana kupata uzoefu wa michuano na watamtegemea
zaidi mfungaji wao bora wa muda wote, Cahill kuongoza safu ya mbele, kiungo
huyo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Everton ameifungia nchi yake jumla ya
magoli 31 katika michezo 67, huku magoli matatu akiwa amefunga katika kombe la
dunia.
Cahill mfungaji wa goli la kwanza la Soccerrose, katika
michuano hiyo hucheza kwa nguvu na kushambulia moja kwa moja, pia ni mtaalamu
wa kucheza mipira ya juu, kwasasa hucheza zaidi katika nafasi na mashambulizi,
japo wakati mwingine hucheza kama kiungo wa kati, kiungo wa mashambulizi au
mshambuliaji wa pili. Tim, alifunga magoli matatu katika fainali za Ujerumani
wakati, nchi yake ilipoichapa, Japan katika mchezo wa kwanza katika kundi
ambalo walipangwa pamoja na Brazil, Japan na Croatia. Chini ya kocha, Mdachi,
Guus Hiddink timu hiyo ilifanikiwa kuvuka kundi hilo.
Ilifungwa na Brazil katika mchezo wa pili, kabla ya
kulazimisha sare ya kufungana magoli 2-2 na Croatia. Katika hali ya utata
walitolewa na Italia katika hatua ya 16 baada ya kulala kwa goli 1-0 ndani ya
dakika 120. Walirudi tena katika fainali za miaka minne iliyopita nchini,
Afrika na kuishia hatua ya makundi. Walichapwa magoli 4-0 na Ujerumani katika
mchezo wa kwanza, wakalazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Ghana, na kuifunga, Serbia
magoli 2-1 katika mchezo wa mwisho.
Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ilifanya mabingwa
hao mara nne wa zamani wa bara la Asia, kurudi nyumbani kwani, Ghana waliungana
na Ujerumani kufuzu kwa hatua ya pili baada ya kuwa na wastani mzuri wa magoli.
Je, watafanya nini nchini, Brazil katika fainali zao za nne kushiriki. Wataanza
kwa kucheza na Chile, juni 13, kasha watacheza na Uholanzi, juni 18, na
kumaliza michezo yao ya makundi kwa kuwakabili, Hispania, juni 23. Staili yao
ya uchezaji si ya kuzuia, ila ni timu ngumu kuifunga kama wapinzani.
No comments:
Post a Comment