Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzani,
Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo
Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Marekani
nchini Tanzania, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar
es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo.Ikulu,
Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Balozi mpya wa Marekani, Mheshimiwa
Balozi Mark Childress ambaye amefika ofisini kwa mheshimiwa Makamu wa Rais kwa
ajili ya kujitambulisha.
Balozi Childress alimueleza Mheshimiwa Mkamu wa Rais kuwa,
Tanzania ni nchi yenye uhusiano maridhawa na Marekani na kwamba katika kipindi
chake kama Balozi atahakikisha uhusiano huu mzuri uliojengwa unadumishwa na
kwamba, nchi hizi mbili zinazidi kuwa na maeneo ya kushirikiana hasa
yanayolenga kuboresha maisha ya watu na kuwapatia maendeleo.
Balozi Childress pia alisema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia
kama mfano kufuatia kuonesha mabadiliko ya haraka katika miradi mbalimbali
inayoendeshwa hapa nchini kwa ushirikiano na watu wa Marekani na akafafanua
kuwa, kazi iliyoko mbele ni kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua zaidi na
sio kurudi nyuma.“Mheshimiwa Makamu wa Rais, kila nikipata fursa ya kukutana na
wenzangu tumekuwa tukizungumzia suala la Tanzania kupiga hatua kwa haraka. Mna
mambo mengi yaliyofanyika na kazi iliyopo ni kuendelea kupiga hatua pasipo
kurudi nyuma,” alisema.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi
Childress kuwa, Tanzania ipo katika kipindi ambacho kinaonesha mabadiliko
makubwa ya kiuchumi na kwamba kazi ya serikali ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa
uchumi unakuwa na unasaidia vizazi vya sasa na vijavyo.
“Mtazamo wetu katika serikali ni kuwa Tanzania itapiga hatua
kubwa katika miaka michache ijayo. Lengo letu ni kutazama kuwa ukuaji wa uchumi
hauwi wa muda mfupi, tunatazama pia maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Kuhusu suala la utunzaji mazingira, Balozi Childress alisifu
hatua za Mheshimiwa Makamu wa Rais hasa katika kazi ya uhamasishaji upandaji
miti na akasema, utunzaji wa mazingira ni jambo la muhimu ili kuifanya nchi
yetu iweze kuendelea na isikabiliane na matatizo yanayotokana na mazingira
kuharibiwa.
“Nakupongeza Mheshimiwa Makamu kwa kazi yako ya uhamasishaji
utunzaji wa Mazingira. Usichoke kufanya hivyo maana unasaidia dunia,” Balozi
Childress alisema.
Imetolewa na : Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment