Mashuhuda wa ajali hiyo wakitoa msaada wa kulinyanua akiwemo Mh Mwigulu Nchemba |
Gari aina ya RAV4 ikiwa imeshainuliwa tayari na Majeruhi wametoka walikuwa wawili.
Kazi ya Kuondoa Betri ya Gari ndio inafanyika ilikuepusha Moto |
Ajali ndogo Imetokea maeneo ya Kibaigwa ikihusisha gari aina
ya RAV4 iliyokuwa ikitokea Mkoani Morogoro kwenda Dodoma,Ajali hiyo mbayo
haijasababisha Kifo chochote imetokea majira ya Mchana na Sababu ya ajali
inatajwa kuwa ni Mwendo kasi wa Dereva na hatimaye Gari Kumshinda na kupinduka.
Katika hali ya Kuonesha Ubinadamu na Utu kwa Watu
Wengine,Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa akitoka Dodoma kuelekea Morogoro kwenye
Mkutano alilazimika Kusimama kwa Muda kwenye ajali hiyo kwaajili ya Kutoka
Huduma ya Kwanza kwa Majeruhi kama anavyoonekana Pichani hapo Juu.Jambo hilo
liliwafurahisha sana Wananchi waliokuwa eneo la ajali na waliomba Viongozi
wengine waige tabia hii ya Mwigulu Nchemba ya Kushirikiana na Wananchi wakati
wa Shida husuasani wanapoona ajali barabarani,Ugonjwa,Misiba n.k wajitahidi
kutoa Ushirikiano.
Picha/Maelezo na Sanga Jr.
No comments:
Post a Comment