Utabakia Stevie? Hodgson ana matumaini ya kutompoteza
Gerrard
ROY Hodgson atajaribu
kumshawishi Steven Gerrard ili aendelee
kucheza soka la kimataifa mpaka 2016.Nyota huyo amebaki njia panda juu ya
hatima ya soka lake la kimataifa kutokana na matokeo mabaya ya kombe la dunia,
lakini bado anahitajika na klabu yake ya Liverpool itakayoshiriki michuano ya
UEFA msimu ujao.Japokuwa Gerrard, 34, ameshindwa kutamba kombe la dunia,
thamani yake na uzoefu wake unahitaji katika kikosi cha England na Hodgson anatamani kuona anaendelea kucheza
licha ya vijana wengu kuchipukia kwasasa.
Frank Lampard anajiandaa kustaafu soka la kimataifa, kwahiyo
Gerrard atabaki mchezaji pekee mkongwe na England haitaki kumpoteza kwasababu
anawaunganisha vijana katika kikosi hicho.
Luis Suarez akimpa
pole Gerrard baada ya kufanya vibaya
kombe la dunia
Hata hivyo, Gerrard ataifikiria klabu yake ambayo ina mechi
ngumu msimu ujao baada ya kufuzu UEFA.
Gerrard amesema atafanya maamuzi baada ya kuzungumza na
marafiki, familia na kocha wa Liverpool,
Brendan Rodgers baada ya kombe la dunia.Mawazo Rodgers yatakuwa muhimu
zaidi na inaonekana kocha wa Liverpool na madaktari wa timu watapenda kumpa
mapumziko Gerrard baada ya kombe la dunia.Hata kama mwenyekiti wa FA ,
Greg Dyke amemhakikishia kazi Hodgson mpaka 2016 licha ya kuchemsha
kombe la dunia, mechi ya mwisho dhidi ya Costa Rica itakuwa muhimu sana na kama
England itapoteza, kocha huyo atakuwa katika mazingira mabaya.
No comments:
Post a Comment