Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 3, 2014

MAITI AKUTWA AKIELEA MACHIMBO YA KOKOTO TEMEKE


Maiti  mwanamume aliyetambulika kwa jina la Hussein Seif (40) amekutwa akielea kwenye mashimo ya machimbo ya kokoto, Wilaya ya Temeke.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema, maiti huyo alikutwa katika eneo la Saranga, Mji Mwema, Kigamboni, juzi saa 12 jioni.
Alisema alikutwa akielea kwenye machimbo hayo bila kuwa na jeraha lolote. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mara ya mwisho Seif alifika nyumbani kwa mdogo wake aitwaye Seif Msaki akitokea kwake Kimanzichana.



Kwa mujibu wa Polisi, baada ya muda mfupi aliaga anaenda kutembea na tangu hapo hakuonekana mpaka maiti alipokutwa maeneo hayo. Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, maiti amehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni na upelelezi unaendelea.
Katika tukio jingine, mtembea kwa miguu aliyetambuliwa kwa jina la Mbaraka Amiri (28) amekufa baada ya kukanyagwa na gari akivuka barabara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema ajali hiyo imetokea juzi saa 10 jioni katika Barabara ya Pugu, eneo la Kituo cha daladala cha Mzambarauni.
Alisema gari lililosababisha kifo hicho ni Toyota DCM lenye namba T564 ANA, lililokuwa likiendeshwa na Khamis Kanyamala (34). Lilikuwa likitokea Gongo la Mboto kwenda Mombasa na lilipofika eneo hilo Amiri alijaribu kudandia wakati likiondoka ndipo aliteleza na kukanyagwa na tairi za nyuma za gari hilo.

No comments:

Post a Comment