Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka
1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri
wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad
Wilson Ngewe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti
wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.
Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia
usafiri wa Nchi kavu na Majini Tanzania.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment