Mwili wa marehemu Yasin Jailan (15) aliyekata roho ndani ya
wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro huku dokta akizichapa
kavukavu.
Akiwa mitaani akisaka matukio, mwanahabari wetu alivutiwa
waya na chanzo chetu kisha akatonywa kuwa kuna bonge la timbwili kwenye wodi
namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya
Timbwili! Katika hali ya kusikitisha mgonjwa Yasin Jailan
(15) aliyekuwa wodini anadaiwa kukata roho huku dokta akizichapa kavukavu na
wagonjwa, Ijumaa Wikienda limenasa kisa cha ajabuMorogoro ambapo alitii wito na
kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri (huwa Global hatulazi damu kufika
eneo la tukio).
Alipofika wodini hapo, mwandishi wetu alishuhudia mtoto
akikata roho huku baba mwenye mgonjwa aliyetajwa kwa jina la Jailan Mrisho
akizichapa na daktari ambaye jina halikupatikana.
Baba wa marehemu (kushoto) akilia kwa uchungu.
Kwa mujibu wa baba mwenye mgonjwa, alimfikisha mwanaye
hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria uliokuwa umepanda kichwani
na kusababisha kuanguka ovyo.
Alidai kuwa baada ya vipimo vya mwanaye walishauriwa kwenda
kununua dawa ambazo ziliwagharimu shilingi elfu arobaini.
Alisema walipofanikiwa kupata fedha na kununua dawa hizo,
daktari alidaiwa kumuuzia mgonjwa mwingine hivyo kusababisha timbwili hilo.
Dada wa marehemu naye akiwa hospitalini hapo.
Baada ya kuona hali tete huku watu wakiwa na hasira
wakimlalamikia daktari huyo kwa uzembe, mwanahabari wetu alipiga simu kituo
kikuu cha polisi mkoani hapa ambapo polisi wa pikipiki almaarufu kama tigo
walifika na kumchukua daktari huyo kisha kumkimbiza kituoni kumnusuru na kipiga
kutoka kwa watu wengine ambao walifika hospitalini hapo kuwaona wagonjwa wao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, John Laswai
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi baada ya kumnusuru dokta huyo ambaye kwa sasa anadunda mtaani.
Baadhi wanachi waliojaa hospitalini kushuhudia mkasa huo.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mipango ya mazishi ya
marehemu ilikuwa ikifanyika nyumbani kwao maeneo ya Mkuyuni mkoani hapa.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kwamba kumekuwa na
vifo vingi vinavyosababishwa na madaktari ambao hawana wito wa kazi hiyo hivyo
serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii chini ya waziri wake, Dk.
Seif Selema Rashid kuchukua hatua juu ya suala hilo.
Daktari akikimbizwa kituo cha polisi ili kuepushwa na kipigo
kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.PICHANA GPL

No comments:
Post a Comment