skip to main |
skip to sidebar
ADEBAYOR KUKOSA ZIARA YA MAREKANI NA TOTTENHAM BAADA YA KUUMWA MALARIA
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor atakosa ziara ya Marekani baada ya kuukutwa na Malaria.
Adebayor, 30, alilazwa hospitali siku ya Jumamosi kwa kile klabu yake imesema "homa ndogo" ya malaria.
Alitarajiwa kutoka hospitali siku ya Jumatatu, lakini hataweza kurejea mazoezini hadi baada ya wiki moja.
"Vipimo vya mapema vimeonesha ugonjwa upo katika ngazi ya chini, na matibabu yanafanya kazi" imesema taarifa ya Tottenham.
Spurs wataanza ziara yao ya mechi za kabla ya msimu dhidi ya Seattle
Sounders Julai 19, kabla ya kucheza na Toronto FC na Chicago Fire.
Mchezo wao kwa kwanza wa ligi utakuwa dhidi ya West Ham, Agosti 16.
Adebayor, aliyewahi kuichezea Arsenal, Manchester City na Real Madrid, alifunga magoli 14 msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment