Na Steven Augustino, Tunduru
POLISI Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma walilazimika kutumia Mabomu na
risasi za moto kwa wingi ili kuwanusuru Askari wake wawili wasiuwawe
katika mzozo uliotokea July 11 mwaka huu kati yao na Wananchi wa
Vijiji vya Lukumbule na Mchesi.
Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa mkasa huo ulitokea katika
Kitongoji cha Silaju kilichopo katika Kijiji cha Mchesi huku chanzo
cha Mzozo huo kikidaiwa kusababishwa na Polisi hao, baada ya kumzuwia
mwendesha pikipiki aliyetambulika kwa Jina la Sijaona Alli (Feruzi)
(31) kwa lengo la kumtaka asimame iliawapatie chochote (rushwa) kama
ilivyozoeleka na Polisi wa jeshi hilo hapa nchini.
Sambamba na uharibifu huo pia Wananchi hao waliwajeruhi Polisi wawili
baada ya kuwashambulia kwa kuwapiga kwa mawe zikiwa ni juhudi za
Wananchi hao kupinga vitendo vya uonevu wa polisi hao ambao
waliwatuhumu kuwanyanyasa kila siku kwa kukamata na kuwatoza fedha
waendesha pikipiki na baiskeli Kijijini hapo.
Kufuatia vurugu hizo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo
ililazimika kuongeza vikosi vya polisi katika eneo la kijiji hicho ilikuwanusuru Vijana hao waliotajwa kwa majina ya namba ,G1921 PC. Chale
na H,9239 Pc Benjamini.
Wakisimulia mkasa huo baadhi ya mashuda wa tukio hilo walidai kuwa
baada ya Polisi hao kumzuwia mwendesha pikipiki huyo asipite huku
akiwa katika mwendo kasi aliwagonga na kuwaumiza vibaya hali ambayo
iliyopelekea Wananchi wa Vijiji vya Lukumbule na Mchesi Kuchukizwa na
kitendo hicho baada ya kukitafsiri na kuamini kuwa ni Uonevu.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Diwani wa kata ya Lukumbule Bw Issa
Kitumbi na watendaji wa Vijiji vya Mchesi Bw Ali Mnandi na Omari Chowo
wa Lukumbule walisema kuwa vurugu zilianza kujitokeza katika Zahanati
ya kata hiyo baada ya Wananchi kupeana taarifa juu ya tukio hilo hali
ambayo ilimfanya muuguzi wa kituo hicho kuwafungia ndani Polisi na
majeruhi hao na kupiga simu kituo kikuu cha polisi Tunduru ili kuomba
msaada wa kuwanusuru polisi wasishambuliwe na Wananchi hao.
Akiongea kwa taabu majeruhi Sijaona Alli (Feruzi) ambaye amelazwa
kitanda namba 16 katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru kwa matibabu
alisema kuwa alikumbwa na mkasa huo wakati akirejea kutoka shambani
ambako alienda kupulizia mikorosho yake na kwamba alisimamishwa ghafla
katika eneo la kona.
Aliendelea kueleza kuwa wakati akijaribu kupunguza mwendo kwa
kurudisha gia ili asimame ghafla pikipiki yake namba T823 Cfrilipigwa teke na askari aliyemtaja kwa jila moja la PC Benjamini na
kujikuta anaanguka na kuumia.
“Nilikuwa natoka shambani kupulizia mikorosho yangu ghafla
nikasimamishwa eneo la kona iliyopo katika Mtaa wa Silaju, lakini
wakati najiandaa kusimama pikipiki yangu ilipigwa teke na kunifanya
nikose balansi na kuangua” alisema Feruzi.
Feruzi aliendelea kueleza kuwa kutokana na yeye kuwa na mahusiano
mazuri na baadhi ya polisi katika kituo hicho amekuwa akisimama na
kuzungumza nao kila anapo simamishwa nao na akaongeza kuwa wiki moja
iliyopita polisi hao walimkamata na kumtoza faini ya shilingi 60,000/=
kisha kumpatia kibali cha kutomkamata tena hali ambayo ilimfanya
aonekane kutokuwa na uhasama wala mashaka nao tena.
Akizungumzia mkasa huo Kaka wa majeruhi huyo Bw. Said Alli aliwaomba
Viongozi wa jeshi hilo kumsaidia ndugu yake kwa kutenda haki, kwani
Polisi wa ngazi ya chini wameanza kumtishia ndugu yake kuwa watamkata
miguu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Msikhela Mihayo amethibitishakuwepo kwa tukio hilo la mapigano kati ya Polisi na Wananchi hao pia
walichoma moto pikipiki yenye namba za usajili T 342 CEX aina ya SNLG
ambayo mali ya askari polisi No,H 925 PC Benjamini ,mtambo wa
kufulia umeme jua (SORLA) ,Madirisha mawili,Televisheni pamoja na kung’oa paa
la kituo hicho.
Kamanda Msikhela aliendelea kufafanua kuwa kufuatia tukio hilo mpaka
sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa licha ya kuwa kikosi maalumu cha
polisi toka polisi mkoa ambacho kinaongozwa na afisa upelelezi wa
makosa ya jinai ya mkoa Bw. Revokatus Malimi kimeshapelekwa na
kinaendelea kuwasaka watuhumiwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake .
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya mkuu wa Wilaya ya
Tunduru Chande Nalicho pamoja na kukiri kuwepo kwaa tukio hilo
alieleza kuwa hali kwa hivi sasa katika kijiji hicho ni shwari na hivi
sasa wapo kwenye kikao cha Ulinzi na usalama kufanya tathimini ya
hasara iliyotokea.
No comments:
Post a Comment