Klabu ya Young Africans haijajitoa kushiriki mashindano ya
Kombe la Kagame chini Rwanda kama inavyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya
habari nchini na kusema taarifa hizo ni za uongo.
Katibu mkuu wa Yanga SC Bw Beno Njovu amesema
taarifa hizo
zilizosambazwa ni za uongo na kuwa kwa siku ya leo hajaongea na mwandishi wa
habari yoyote juu ya michuano hiyo.
Sie hatujatangaza kutoshiriki michuano ya Kagame, kama
tulivyosema awali kikubwa tunasubiri taarifa rasmi za kushiriki kutoka CECAFA
zitufikie ofisini nasi tupange mikakati yetu "amesema Beno".
No comments:
Post a Comment