Wakazi 30 wa Kijiji cha Kegonga Kata ya Nyanungu Tarafa ya Ingwe Wilayani Tarime
Mkoa wa Mara, wamedai kuwa wanadai fidia ya zaidi ya Sh milioni 100 kutokana na mifugo yao kuuawa.
Wanadai mifugo hao waliuawa na baadhi ya askari waliotekeleza Operesheni Tokomeza Ujangili.
Wakazi hao ni wale wanaoishi jirani na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Walitoa madai hayo kwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, Nyambari Nyangwine. Walidai wanamuomba awape msaada ili Serikali iweze kuwapa fidia ya ng'ombe 500, punda 36, mbuzi 80 na kondoo 19, waliouawa katika operesheni hiyo mwaka jana.
Walitoa malalamiko yao kwa Nyangwine katika mikutano mitatu ya hadhara, iliyofanyika katika kata za Nyanungu na Goronga.
Wakazi wa kata hizo, Mwita Marwa, Nyamhanga Wambura na Masero Chacha, walidai wanaotakiwa kulipwa fidia hiyo ni wafugaji na wakazi wa vijiji vya Kegonga, Mangucha, Nyarukoba , Kitawasi, Itiryo na Nyanungu, jirani na Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa upande wa Tarime.
“Tunakuomba Mbunge wetu utufikishie kilio chetu kwa viongozi wa juu ili tuweze kufidiwa mifugo yetu hiyo iliyouawa, " walisema wananchi hao.
Walidai wameishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 100 , lakini hawajapata tatizo kubwa, kama hilo la mifugo kuuawa.
Kwa upande wake, Nyangwine alisema "Malalamiko yenu nimeyapokea, nilipokuwa bungeni niliuliza masuala haya na Serikali imeunda Tume kuja hapa katika vijiji vilivyokumbwa na matatizo haya ya kuuawa mifugo wakati wa Operesheni Tokomeza.
Ninachowaomba ninyi wananchi mnatakiwa kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tume hiyo itakapofika hapa kuchukua malalamiko yenu, muwe wawazi na wakweli ili madai yenu haya yaweze kufanyiwa kazi”.
Aliwataka waache kuwasikiliza wanasiasa, wanaotaka kuwachochea kwa lengo la kutafuta umaarufu usio na msingi. Alionya kuwa kuwasikiliza wanasiasa, kutahatarisha haki zao.

No comments:
Post a Comment