Ahadi
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa
wasanii wa Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi na weledi wao kwa
kuwaandalia mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa sanaa kutoka Marekani sasa
imetimia.
Terrence |
Akizindua
Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na Muungano wa Wasanii Tanzania
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi uliopita, Juni 14, 2014, Rais
Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango cha usanii na weledi wa wasanii wa
Tanzania kwa kusaidia kuandaa mafunzo yatakayoendeshwa na wasanii maarufu
kutoka Marekani.
Chaka Zulu |
Katika
kutimiza ahadi hiyo ya Rais Kikwete, kundi la wasanii kutoka Marekani
limewasili nchini usiku wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya kuendesha
mafunzo hayo yanayofanyika keshokutwa, Jumatatu, Julai 14, 2014, kwenye Ukumbi
wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mjini Dar es Salaam. Kiasi cha wasanii 250
wamealikwa kushiriki semina hiyo inayoitwa Mafunzo ya Uendelezaji Usanii.
Banner |
Wasanii
ambao wako nchini kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo ni Chaka Zulu, Mtendaji
wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis
Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki
ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Wengine
ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni
ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton,
Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.
Mbali
na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo wamekuwa wakizifanya kwa
makundi madogo madogo tokea walipowasili nchini, pia wanamuziki hao wa Marekani
na kundi la wapiga picha watatembelea sehemu mbali mbali nchini ambako watapiga picha na kuandaa
vipindi vya kuitangaza Tanzania katika vyombo vya habari vya Marekani.
Imetolewa
na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12
Julai,2014
No comments:
Post a Comment