Kwenye Kituo cha
Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala, Dar kuna faili la kesi namba MBL/RB/
9817/2014- KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI ambalo linamsaka kijana Juma Athumani
(30), mkazi wa Charambe, Mbagala kwa kosa la ubakaji wa denti wa darasa la
saba. Habari za kiintelijensia zilidai
kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ni muuza
genge, alitenda kosa hilo Agosti, mwaka huu ambapo denti huyo alikuwa ametumwa
na mama yake gengeni.Ilisemekana kwamba jamaa huyo alimuomba denti huyo
wazungumze kidogo ndipo akampeleka gesti kwa lazima.
Akizungumza na gazeti hili bora la habari za mastaa na
kijamii, denti huyo alisema kuwa alipofika gesti, jamaa huyo alilipa fasta na
kumvutia chumbani ambapo alianza kumshika ‘manido’ kisha akamtupia kitandani na
kumwingilia kimwili bila ridhaa yake.
Mama wa mwanafunzi aliyebakwa.
Alisema kwamba, jamaa
alipomaliza shida zake, alimpa buku tano (5,000/=) lakini alipokataa huku
akilia ndipo mwanaume huyo akamuongezea hadi ikafika buku kumi (10,000/=).
“Niliporudi nyumbani mama aliniuliza kwa nini nimechelewa
kisha akaziona hela, akaniuliza nimezipata wapi, nikamwambia amenipa Juma ndiyo
tukaenda hadi gengeni kwa Juma kuuliza ndiyo mama akagundua kuwa nimebakwa.
“Baadaye mama alikwenda kuripoti polisi ndipo Juma
akakamatwa na mimi nikapelekwa hospitali na kugundulika kweli nilikuwa
nimebakwa,” alisema denti huyo.
Habari zilizotufikia punde kabla ya kuingia mitamboni
zilidai kwamba uchunguzi wa polisi unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment