Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto
cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani
mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK
RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu
kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.
Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa
kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.
No comments:
Post a Comment