Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 24, 2014

Makampuni 130 China yatengeneza vifaa vya mateso

 Makampuni nchini China yameingia katika shutuma kali kua wanatengeza na kusafirisha vifaa vya mateso kwa vikosi vya polisi duniani.
Shirika la kutetea haki za binaadamu Amnesty International limetoa taarifa kuwa makampuni yapatayo mia moja na thelathini nchini humo,kati yao wamekiri kutengeneza vifaa hivyo ikiwemo vibanio vya umeme,viti vya umeme,na pingu za vidole gumba.

Inasemekana vifaa vingi japo hutengenezwa na kusafirishwa,vingi matumizi yake ni katika kuleta maumivu mwilini na mateso.shirika hilo la kutetea 



haki za binadamu lina shaka na nchi zenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu hasa Africa na Kusini Mashariki mwa Asia wao ndio wateja wakuu wa vifaa hivyo.

No comments:

Post a Comment