Jalada namba
KW/RB/7565/2014-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI lililopo kwenye Kituo cha Polisi cha
Kawe, Dar, linamhusu mama aliyetajwa kwa jina
moja la Teddy, mkazi wa Tegeta
kwa madai ya kumtumikisha na kumtesa mtoto Magdalena Elisha (10) na
kumsababishia majeraha na makovu ya vidonda sehemu mbalimbali mwilini.
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zilidai kwamba, Teddy
alimchukuwa mtoto huyo jijini Arusha kwa lengo la kumsaidia kukaa na mwanaye
kwa kuwa familia ya mtoto huyo haina uwezo na ameishia darasa la tatu kwa
kukosa vifaa vya shule.
Mtoto Magdalena Elisha anayedaiwa kusulubiwa na mama huyo.
Kwa mujibu wa Teddy,
bila kujua kwamba ni kosa kumwajiri mtoto, aliamua kumwadhibu mtoto huyo
kutokana na kutomsikiliza bosi wake hasa alipokuwa akionywa kuachana na tabia
ambayo haikuwa ikimfurahisha.
No comments:
Post a Comment