Mafuriko katika eneo la Kashmir
Mafuriko yamewaua zaidi ya watu 200 nchini India na Pakistan
huku watabiri wa hali ya hewa wakisema kuwa mvua zaidi inatarajiwa kunyesha.
Majeshi ya mataifa yote mawili yanaongoza shughuli za
uokoaji kwa kutumia ndege ili kujaribu kuyafikia
maeneo ya vijijini.
Takriban watu 100 wamefariki katika eneo la kashmir
linalosimamiwa na India baada ya mafuriko hayo kuyasomba makaazi mbali na
kusababisha maporomoko.
Maafisa katika eneo la kashmir linalosimamiwa na Pakistan
wamesema kuwa takriban watu 110 waliuawa.
Ni mafuriko mabaya kutokea katika eneo hilo kwa kipindi cha
miaka sitini baada ya kuwashangaza raia waliodhani kwamba msimu wa kila mwaka
wa upepo mkali ulikuwa umekwisha.


No comments:
Post a Comment