Mbunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar na Mwenyekiti wa Baraza
la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Halima James Mdee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii mwishomi mwa wiki
iliyopita, Mdee licha ya kuponda utendaji kazi mbovu wa serikali kuhusu
mahabusu, aliyataja mambo hayo kama ifuatavyo:
HAUSIGELI NA KESI NDOGONDOGO
Alisema alipofika mahabusu aliwakuta wasichana wadogo ambao
baadhi yao ni mahausigeli wakamlalamikia kwamba wamekaa ndani kwa muda mrefu
bila kesi zao kusikilizwa.
Alisema kwa uchunguzi wake alibaini kuwa wasichana
hao wa
kazi za ndani, kesi zao zilifunguliwa kwa kubambikwa na mabosi wao pale
wanapodai malipo, hivyo wao husingiziwa wizi au kosa lolote.
UBOVU WA CHAKULA
Pia Mdee alisema chakula cha mahabusu hakiridhishi kutokana
na kupikwa bila kiwango na kuwa na michanga, wakati mwingine hakiivi.
MAHABUSU KUKAA MUDA MREFU BILA KESI KUSIKILIZWA
Jambo jingine alilodai kukumbana nalo Segerea ni mahabusu
kukaa kwa muda mrefu kati ya miaka 4 hadi 7 bila kesi zao kusikilizwa kwa
kisingizio cha upelelezi kutokamilika.
MACHANGUDOA KUWASHAWISHI MABINTI
Katika sakata lingine, Mdee alisema wanawake wengi
waliokamatwa kwa makosa ya kujiuza usiku (machangu) wanaopelekwa mahabusu
wamekuwa wakiwashawishi wasichana wadogo, hasa mahausigeli wanaofikishwa humo.
“Wasichana hao huwashawishi mahausigeli kiasi kwamba
wanapotoka mle mahabusu na wao wanakwenda kujihusisha na ukahaba na biashara ya
madawa ya kulevya kwa vile baada ya kutoka hawapewi nafasi na mabosi wao
kuendelea na kazi,” alisema Mdee.
MAHABUSU WA KIKE KUADHIBIWA NA ASKARI WA KIUME
Jambo lingine aliloligundua Mheshimiwa Mdee ni kitendo cha
askari wa kiume kutoa adhabu kwa maabusu wa kike badala ya kuadhibiwa na
wanawake wenzao kitendo ambacho alisema kimekuwa kikiwadhalilisha mahabusu hao.
Hata hinyo, Mdee alimuomba Waziri wa Sheria na Katiba,
Asharose Migiro kuanzisha utaratibu wa safari za kushtukiza magerezani na
kuzungumza na mahabusu ili kusikiliza kero zao na kuzitatua.
Jumanne iliyopita, Mdee alifikishwa katika gereza hilo saa
11 jioni ambako alilala hadi kesho yake saa 1 asubuhi kwa madai ya kufanya
maandamano haramu kwenda Ikulu ya Dar.
No comments:
Post a Comment