Mahakama hiyo imefutilia mbali uamuzi wa mahakama ndogo
inayozitaka hospitali za serikali kutumia kiwango kikubwa cha pesa kupandisha
daraja hospitali zao na kuongeza huduma za kutoa mimba.
Mahakama hiyo ndogo ingali inatathmini uhalali wa sheria
hiyo iliyotiwa saini na gavana Rick Perry mnamo mwaka 2013.
Uamuzi huo una maana kuwa kliniki nyingi zilizofungwa ambako
wanaweza walikuwa wakitolea mimba zinaweza kufunguliwa upya, hatua ambayo
imepongezwa na wanaharakati wanaopigia debe swala la kutoa mimba.
"tuna afueni maana mahakama iliingilia swala hili na
kufutilia mbali sheria hiyo, na tunatumai kuwa sheria hii hatari inaweza
kufutiliwa mbali kabisa,'' alisema Cecile Richards, mkuu wa shirikisho la uzazi
wa mpango nchini Marekani.
Ikiwa sheria hio ingepitishwa, kliniki nane za kutoa mimba
zingefungwa katika jimbo hilo la pili katika wingi wa idadi ya watu nchini
Marekani.
Kati ya majaji wanane wa mahakama ya juu zaidi, sita
waliunga mkono haki za wanaotaka kuhalalisha utoaji mimba.
Wanasiasa wenye msimamo mkali wa chama cha Conservative
wanasema kuwa sheria hiyo inalenga kuwalinda wanawake lakini wakosoaji wake wanasema
kuwa sheria yenyewe ni njama ya kuharamisha utoaji mimba, ambayo ni haki
inayopewa na katiba ya nchi tangu mwaka 1973.
Mnamo mwezi Agosti, jaji mmoja kwa jina Lee Yeakel, alisema
kuwa sheria hiyo hailengi kuhakikisha kuwa wanawake wanakuwa salama bali
kudhibiti huduma za utoaji mimba katika jimbo hilo.
Nyingi ya kliniki za kutoa mimba zimefungwa kutokana na
sheria hiyo ambayo inasema madaktari ambao kazi yao ni kutoa mimba wasiruhusiwe
kuendesha shughuli zao katika hiospitali nyingi.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment