Marubani walioasi jeshi la Iraq na kujiunga na kundi la
wapiganaji wa Islamic State wameanza kutoa mafunzo ya urubani kwa wapiganaji IS
nchini humo.
Marubani hao wanatumia ndege tatu za kivita walizoziteka
kutoka kwa jeshi. Hii ni kwa mujibu wa kundi moja wa kutetea haki za binadamu
la nchini Uingereza ambalo linafuatilia mgogoro huo.
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria, (SOHR)
linasema mashahidi wanasema waliona
ndege hizo zikiruka katika uwanja wa ndege
wa kijeshi mjini Aleppo.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Iraq wamefanya mashambulizi
dhidi ya kambi za wapiganaji wa IS karibu na mji wa Tikrit.
Mji huo ni miongoni mwa maeneo mengine ya Syria na Iraq
yaliyotekwa na kundi hilo la IS mwaka huu.
Rami Abdul Rahman,mkuu wa kundi la SOHR, amesema kuwa
wapiganaji wa IS wanatumia wanajeshi wa Iraq waliokuwa wanajeshi chini ya utawala
wa Saddam Hussein kutoa mafunzo kwa wapiganaji nchini Syria.
Haijulikani idadi ya wanajeshi wa jeshi la Iraq walioasi
jeshi.
Waliozishuhudia ndege hizo waliambia shirika la SOHR kwamba
ndege hizo zilikuwa aina ya MiG-21 au MiG-23.
Mwandishi wa BBC mjini Baghdad, Sally Nabil ameambia IS
kwamba ndege tatu zilitekwa na wapiganaji wa IS kutoka kwa jeshi la Syria mjini
Aleppo na Raqqa.
Mji wa Aleppo uligeuka na kuwa kitovu cha mapigano kati ya
wapiganaji wa Syria ambao sasa wanajumuisha wapiganaji wa IS na wanajeshi wa
serikali baada ya harakati za kumuondoa mamlakani Rais Bashar al-Assad kuanza
mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment