Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 18, 2014

PICHA::DANGURO LINGINE HATARI LAFUMULIWA SHULENI

 askari wa ulinzi shirikishi, wamefanikiwa kufumua danguro hatari linaloendesha shughuli zake katika eneo la shule baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni mke wa mtu akifanya uzinzi na njemba ambaye hakujulikana jina lake. Kikosi cha OFM kimkurupusha mke wa mtu aliyekuwa akifanya uzinzi na njemba moja(jina halikufamika). Tukio hilo la aibu ya karne lilijiri ndani ya eneo la shule ya msingi Shekilango, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar, hivi karibuni ambapo mke huyo wa mtu alikuwa akichepuka. Awali, OFM ilipokea taarifa za kuwepo kwa uchafu huo kutoka kwa wasamaria wema wanaoishi eneo hilo baada ya kukerwa na tabia hiyo chafu huku wakiacha kondom zikiwa zimezagaa na kuhatarisha afya za watoto wao ambao huchezea mipira hiyo ya kinga kama mapulizo.
Baada ya OFM kunyetishiwa ishu hiyo, walishirikiana na askari hao ambapo walivamia eneo hilo na kumbamba mwanamke huyo akibanjuka na njemba.
Wazinifu wakivaa mara baada ya kunaswa wakifanya yao. Wawili hao, baada ya kubambwa 'laivu' walitiwa kizuizini kabla ya vijana wanaodaiwa kuchukua posho kwa wanaofanyia mambo yao kwenye danguro hilo kuanzisha vurumai ingawa walidhibitiwa huku jamaa aliyekuwa anahudumiwa akitoka nduki.



Akizungumza na gazeti hili, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema kwamba kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na kundi la watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema: "Dah! Mngewahi dakika kumi tu, mngemkuta baba wa Kiarabu aliyeingia na mwanamke muda si mrefu, hili danguro linatumiwa usiku kucha, yaani linapoingia giza tu hapa ni balaa hadi asubuhi."

Mwalimu wa zamu, Kilavo Charles, aliiambia OFM kuwa suala hilo limeshafikishwa kituo cha Polisi Mabatini ambao waliahidi kulishughulikia.“Ni aibu, asubuhi watoto wanafagia kondom, tunakosa cha kuwaambia, hii ni hatari kwa kweli na tunaomba mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi jambo hili,” alisema.CHANZO GPL

No comments:

Post a Comment