Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 16, 2014

WAALIMU WAIDAI SERIKALI ZAIDI YA SH.MILIONI 985 KWA MIEZI MIWILI MFULULIZO.


Chama cha waalimu mkoa wa kilimanjaro (CWT) kinaidai serikali zaidi ya shilingi milioni 985 zilizokatwa kwenye mishahara ya waalimu kwa miezi miwili hali iliyochangia vyama saba vya mkoa wa kilimanjaro kushindwa kutoa mikopo  kwa waalimu na kuwafanya watumishi hao kwenda kukopa kwenye taasisi nyingine na kushindwa kurejesha kwa wakati.
 Hayo yamebainishwa na mameneja wa vyama hivyo na kusema kuwa imekuwa kero kubwa kutokanana vyama hivyo kushindwa kutoa mikopo  na hivyo kusababisha baadhi ya walimu kwenda kwenye taasisi nyingine za kifedha kutafuta mikopo kwa ajili ya mahitaji yao.

Wamesema  zaidi ya  walimu 12,000 ambao ni wananchama wa vyama vya akiba na mikopo wamekatwa mishahara yao  na fedha hizo tangu mwezi julai hazijawasilishwa kwenye saccos hizo hali ambayo inaleta usumbufu mkubwa kwa Walimu.
Kwa upande wake katibu wa chama cha walimu CWT mkoa wa kilimanjaro Bw.Nathanael Mwandete ameiomba serikali kuwasilisha fedha hizo kwa wakati kwa kuwa hali hiyo inaweza kuhatarisha  shughuli za ufundishaji  kutokana na walimu hao  kufuatilia madai hayo ambayo ni haki yao.
Naye mwenyekiti wa chama cha waalimu (CWT) mkoa wa kilimanjaro Bw.Omari Mchomvu amesema kama serikali haitalipa madai hayo kwa wakati chama hicho kitahamasisha walimu kuandamana.

CHANZO:  ITV TANZANIA

No comments:

Post a Comment