Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 25, 2014

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KESHO

Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam leo juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaotaraji kuanza leo katika ukumbi wa Karimjee na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho kutwa. 

BALOTELLI RASMI LIVERPOOL


Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli, 24, amekamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda Liverpool kwa pauni milioni 16. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City, amekubali mkataba wa muda mrefu, ingawa hatoweza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani Jumatatu usiku. Balotelli aliondoka City miezi 17 iliyopita baada ya kupachika mabao 30 katika misimu mitatu. 


Mashindano ya FEASSSA yaanza kutimua vumbi


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari za Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA (Federation of East Africa Secondary Schools Sports Association), jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Waziri Maghembe akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Tanki la Maji katika kijiji cha Itege mjini Dodoma


Waziri wa Maji,Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akikagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita million 5.5 kwa ajili ya kuhudumia wakazi wapatao 20,000 katika eneo la Itege mjini Dodoma. Tanki hilo ni miongoni mwa matenki manne yanayoendelea kujengwa. Ujenzi wa mradi huu unajengwa kwa ushirikiano wa Serikali za Tanznia na Jamhuri ya Korea kwa gharama ya Sh. Billion 78. 

UTAFITI: UKIAMBIWA SENTENSI HIZI NA MWANADADA UJUE ANAKUDANGANYA


1.Ungejua wala sina haraka ya kuolewa!
Hakuna mwanamke ambaye yuko tayari kuona umri unamkimbia, ameshahudhuria harusi za marafiki zake, pengine ameshaliona mpaka gauni litakalompendeza harusini halafu eti akuambie hana haraka ya kuolewa!

2. Ngoja Nikavae, nipe dakika tano tu!

Ukiambiwa hivi, basi Kama hujanywa soda muda mrefu huu ndo muda muafaka! Tafuta sehemu yenye utulivu upate kinywaji chako maana hizo dakika tano ni dakika hamsini!

3.Wala sioni  wivu ukiwa unawaangalia wanawake wengine

Akikuambia hivi, anataka tu akuonyeshe ni jinsi gani amekua kiakili, na ni mtu muelewa saana.. lakini moyoni mwake anatamani kukupiga makofi unapomuangalia msichana mwingine huku akijiuliza moyoni,  kwani huyo anaemuangalia amenishinda nini?


4.Hata kama unapata mshahala mdogo, mi nimeridhika kabisaa.. (mmmh Kweli?)

5.Mbona dada yako hajaja kututembelea muda mrefu? Nime”mmiss” sana!
Mara chache sana kutakuwepo na  upendo kati ya mpenzi wako na dada yako au hata mama. Kwa mwanamke ni  bora umletee  wadogo zako wa kiume kumi nyumbani atawalea ila sio dada yako mmoja!


Picha: Rihanna alipojikuta anatazama game ya Basketball ambayo Chris Brown alicheza

 Riri alikaa viti vya mbele kabisa akitazama game ambayo ex wake alikuwa akicheza pia, sasa tazama jinsi Riri alivyonuna na kujaribu kukwepa kumtazama Chris kila alipokatiza karibu na alipokaa.
 Riri alitangazwa hadi kwenye flyer kuwa atahudhuria kama mgeni maalum,lakini mwimbaji wa ‘New Flame’, Breezy alitokea kama surprise.
  
Hii ni wiki ambayo pia Karrueche na Chris Brown wamepatana baada ya kuachana kwa muda, na pia Rihanna na Drake wameonekana tena pamoja kwenye club ya usiku baada ya kuzinguana kwa muda pia.


HUU NDIO MKWANJA (PESA) ANAYOLIPWA DIAMOND KWA SASA KWENYE SHOW MOJA

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako.
Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo. 


PICHA ZETU YA SIKU::RAIS KIKWETE ALIPOKUWA ANAPATA SELFIEEE NA GWIJI WA MADRID

a
 Kiungo wa timu ya Real Madrid Legends, Christian Karembeu akichukua picha ya kumbukumbu na Rais Jakaya Kikwete.
Wowwwwwwwwww Ni nzuri Usisahau kunitumia

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

 Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.

TAZAMA PICHA 5 ZA MTOTO WA JAY Z NA BEYONCE AKIMSHUHUDIA MAMA YAKE ALIPOKUWA AKIPIGA SHOW KWENYE TUZO ZA MTV


TAZAMA PICHA 20 ZA TUZO ZA MTV ZILIVYOFANA NA SOMA MAJINA YA WASHINDI WOTE HAPA


KHEDIRA KUSALIA BERNABEU


Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira hatoondoka Bernabeu msimu huu, kwa mujibu wa kocha Carlo Ancelotti.
Khedira, 27, alihusishwa na kuhamia Arsenal na Bayern Munich, baada ya Ancelotti kusema alikataa kusaini mkataba mpya.
"Suala la Khedira limetatuliwa. Atabakia hapa na 

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO



Manchester United wamekamilisha majadiliano na Real Madrid na watalipa pauni milioni 63.9 na kuvunja rekodi ya Uingereza kumnunua winga Angel Di Maria (Sky Sports), mchezaji huyo kutoka Argentina huenda akafikia kuuzwa kwa pauni milioni 72, milioni 60 zikilipwa mwanzo na milioni 12 baadaye (Daily Mirror), Juventus wataanza mazungumzo na Arsenal kuhusu Lukas Podolski. Juventus wanamtaka kwa mkopo 

TAZAMA PICHA BEYONCE NA JAY Z NA MWANAO WALIPANDA JUKWAANI KWENYE TUZO ZA MTV

Beyonce may have come into Sunday night’s Video Music Awards leading the way with eight award nominations, but it was her mysterious yet promised big performance that had everyone talking.
The “Drunk in Love” singer did not disappoint either.
Before the night even began it was announced that Beyonce would be receiving the Michael Jackson Video Vanguard Award for lifetime achievement.

MH;WAZIRI AAMUA KUVUA SUTI NA KUSAIDIA MAJERUHI WA AJALI,PICHA 5 ZIKO HAPA

Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.


Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.

TAZAMA PICHA 4 ZA PAKA MWEUSI ALIYEKATIZA UWANJANI WAKATI BARCELONA INAIPIGA ELCHE GOLI 3 BILA


Paka mweusi akikatiza Uwanja wa Camp Nou janaBARCELONA imeanza vyema La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa Camp Npu usiku wa kuamkia leo.Katika mchezo huo, kiungo wa Barca Javier Mascherano alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kocha mpya Luis Enrique akiiongoza timu kwa mara ya kwanza, alionyesha mwanzo mzuri.
Mchezaji wa timu gani? Paka huyu alisababisha mechi isimame ili kwanza apite

CHRIS BROWN ANUSURIKA KIFO, SUGE KNIGHT AKIJERUHIWA KWA RISASI TUKIO ZIMA LIKO HAPA

Cris Brown akiwa Klabu 1OAK kabla ya vurugu kutokea.

Prodyuza mkongwe, Suge Knight amejeruhiwa tumboni na mkononi katika shambulio hilo


KIJANA MOJA ANUSURIKA KIFO NA MWINGINE AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO WAKIJARIBU KUIBA PIKIPIKI KAHAMA

 Haya twendeni vizuri sasa angali huko kwako ana nguvu huyu mtu hunaona  halivyokaaa
 Baada ya kufikishwa hospital ya wilaya ya kahama kwa matibabu ana baada ya wasamaria wema wakimsaidia nesi kumpeleka kwa dakitali kwa huduma .

KESI YA KIFO CHA KANUMBA SURA MPYA.. ELIZABERTH MICHAEL HALI TETE

Jipya! Baada ya kimya cha muda mrefu, imefichuka kwamba kesi ya kuuawa kwa aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ imechukua sura mpya baada ya kuanza kusikilizwa kimyakimya, Ijumaa Wikienda limenasa kinachoendelea.

HUYU NDIO MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA TOKA CCM ALIYEJIUNGA NA UKAWA

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ali Mohamed Kessy ambaye pia ni Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM) akiwatangazia waandishi wa habari kuunga mkono muundo wa serikali tatu uwepo katika Katiba Mpya, mjini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya bunge hilo, Ummy Mwalimu na Makamu wake, Prof Makame Mbarawa ambao walimwita Kessy kumtaka kukanusha kuhusu taarifa yake ya kuwapo tatizo la akidi kwenye vikao vya 

TAZAMA PICHA NA VIDEO ZA DAKTARI ALIYETENGENEZA VIRUSI VYA UKIMWI.


Kuna hii makala nimeletewa. Sijui kama ilishawahi kuwepo hapa. Ni ndefu kidogo (video) ila kweli inaleta kizunguzungu ukiisikia. Sijui ma Drs mnasemaje juu ya hili swala.
Kumbe Tanzania ndiyo center ya AIDS Africa? Lohhh, nilikuwa sijui. Jitahidini hata msio Madokta msikilize kwani wamelielezea vizuri sana. Ila ukweli hata mie sijui. Na kama ni kweli basi hii ni Weapon of Mass Destruction kubwa kuliko hata Fussion bomb la Mrusi.

VIDEO:

LIGI KUU ENGLAND MANCHESTER UTD YATOKA SARE NA SUNDERLAND



FUSO LAUA MWENDESHA BAISKELI IFAKARA, MOROGORO

Mwili wa marehemu ukiwa eneo la ajali. Pembeni ni baiskeli yake.
Baiskeli ya marehemu ikipakiwa kwenye gari.

AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA COASTER MOROGORO!

Askari wa usalama barabarani wakipima eneo la ajali.

Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa ndani ya gari.

MAKANISA SINGIDA YAONYA MATUSI NA UBAGUZI BUNGENI‏

DSC00479
Askofu wa kanisa la Evanglist Assembels of God Tanzania (E.A.G.T) Singida mjini, John Mafwimbo akizungumza kwenye mkutano wa Injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini Singida.Pamoja na mambo mengi, askofu Mafwimbo amewasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kufanya mambo waliyotumwa na Watanzania na si vinginevyo.
Na Nathaniel Limu, Singida

WABUNGE WA CCM WAUNGURUMA HUKO MTERA MKOANI DODOMA‏

IMG-20140824-WA0005
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiwahutubia wananchi katika kijiji Iringa Mvumi Jimbo la Mtera mkoani Dodoma ambapo Chama cha mapinduzi kimeendelea kuuelimisha umma juu ya masuala ya Maendeleo, utekelezaji wa ilani, maandalizi ya uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa, bunge la katiba na mambo yanayohusu maendeleo ya katika vijiji na wilaya zetu. Pia kuwakumbusha juu ya thamani ya muungano wetu na vipengele muhimu vinavyojadiliwa ndani ya katiba.
IMG-20140824-WA0006
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kutema cheche katika mkutano huo.

MAREHEMU LUCIA KIBUSI AAGWA, BOSTON, MASSACHUSETTS NCHINI MAREKANI‏

Watoto wa marehemu Martin na Steven Kibusi kulia wakiwa kwenye chakula cha pamoja baada ya ibada ya kumbukumbu ya kumuaga mama yao kumalizika kushoto ni marafiki wa karibu na watoto wa marehemu wakiwafariji marafiki zao. Pia familia ya marehemu walitoa shukurani za dhati kwa wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika msiba huu wa mpendwa mama yao na kuwezesha kukusanya $19,000 ili kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania " hatuna cha kuwalipa kitakacholingana na hicho kikubwa mlichoifanyia familia hii ya Kibusi, tunawaoombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie mara dufu"

10 BORA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) WAVAMIA STUDIO ZA TIMES FM 100.5 FM JIJINI DAR ES SALAAM.‏

Waendeshaji wa Kipindi cha Filamu Monata kinachorushwa na Kituo cha Redio cha TIMES FM 100.5 wakiendelea na majukumu katika studio za kituo hiko cha Redio Kilichopo Kawe Jijini Dar Es Salaam wakati wa Kipindi cha Filamu Monata leo wakati washiriki 10 Bora wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) walipotembelea Studio hizo 
Jaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) na Presenta wa Kipindi cha Filamu Monata cha TIMES FM, 100.5 Dar Es Salaam akiendelea na kipindi wakati washiriki 10 bora walipotembelea Kituo hiko leo kwaajili ya Mahojiano na waendeshaji wa Kipindi hiko.
 Mmoja wa Washiriki 10 Bora wa Tanzania Movie Talents (TMT) akijibu maswali kutoka kwa Waendeshaji wa Kipindi cha Filamu Monata kinachorushwa na Kituo cha Redio cha TIMES FM, 100.5 Dar Es Salaam.
Mshiriki Wa Tanzania Movie Talents (TMT) akijibu maswali.

UAMSHO WAFUNGUKA CHA MOTO WALICHOKIPATA LUPANGO


KIONGOZI wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), ametoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi akidai kuwa limewafanyia ukatili kwa kuwapiga, hali inayowafanya baadhi yao wajisaidie damu.

Sheikh Farid alitoa madai hayo jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, wakati kesi ya tuhuma za ugaidi inayowakabili ilipokuwa ikitajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Peter Njike, alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi haujakamilika na wanaomba hati ya kuwachukua washtakiwa saba, akiwamo Sheikh Farid kwa ajili ya mahojiano.