OFM kazini! Kile kitengo maarufu cha Global Publishers cha
Operesheni Fichua Maovu (OFM) mwishoni mwa wiki kilifanikiwa kunasa tukio la
aina yake baada ya kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Joni Simon kunaswa na
kitita cha fedha bandia akitaka kuwekewa katika simu yake ya mkononi kupitia
mtandao wa Tigo Pesa, tukio lililotokea Sinza Afrika Sana jijini Dar.
Polisi wakionyesha fedha bandia alizokamatwa nazo bwana Joni
Simon.
Bwana Joni Simon akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
wa kituo cha Mabatini
Kijitonyama ambao wakiongozwa na Kamanda Rashidi wakaingia eneo la tukio mara
moja lakini walilazimika kutumia bunduki kumtisha ili kumtuliza kijana huyo na
kumtia mbaroni.
Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya mtu mmoja huko
mkoani Mwanza, kukamatwa akiwa na kiasi cha shilingi milioni 400 za Kitanzania,
ambazo pia ni bandia, zilizokusudiwa kuingizwa katika mzunguko wa fedha.
No comments:
Post a Comment