Mfanyabiashara wa mbao Manispaa ya Songea, Emmanuel Moshi
(40), mkazi wa Marangu, mkoani Kilimanjaro amemuua mfanyabiashara mwenzake
aliyetambuliwa kwa jina la Didas Alphonce (64), mkazi wa Kilema Kilimanjaro kwa
kumpasua kichwa kwa shoka, kisha yeye mwenyewe kujinyonga kwa kutumia kamba ya
katani katika stoo ya nyumba waliyokuwa wakiishi.
Inadaiwa kuwa Moshi alichukua uamuzi huo baada ya Alphonce
kumdhulumu zaidi ya Sh87.4 milioni.
Walidai kuwa, Desemba 30 mwaka jana, wafanyabiashara hao
walikuwa wakinywa pombe kwenye Bwalo la Magereza na Moshi alikuwa akilalamika
kudhulumiwa na Didas.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa tangu siku hiyo,
wafanyabiashara hao hawakuonekana tena hadi jana.
Ilidaiwa kuwa, mwenye nyumba huyo alitumia funguo zake za
akiba kufungua nyumba hiyo na kukuta mwili wa mjomba wake ukiwa umepigwa na
shoka na tayari umeanza kuharibika.
Mtu mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi alitoa taarifa
kituo cha polisi na walipofika waliubaini pia mwili wa Moshi aliyejinyonga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai uchunguzi wa awali unaonyesha
wafanyabiashara hao walikuwa wanadaiana pesa.
Alisema Mosha ameacha ujumbe mrefu wa karatasi nne
aliouandika kuhusiana na mauaji hayo.
Ujumbe huo: “Kataeni wadhulumaji kati ya matajiri na
maskini, nimeondoa dhambi kubwa ya dhuluma iliyokuwa ikinitesa ulimwenguni,
wadhulumaji wasifumbiwe macho jamii iniunge mkono kuondoa watu hawa.
“Dhuluma aliyonifanyia mtu huyu imekatisha maisha yangu.”
No comments:
Post a Comment