Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC
Maafisa wa polisi nchini Kenya wameupata mwili wa shahidi
muhimu wa mahakama ya ICC siku chache tu kabla ya kutoa ushahidi wake katika
kesi ya naibu wa rais katika mahakama hiyo.
Ripoti za vyombo vya habari nchini Kenya zinasema kuwa mwili
wa Meshash Yebei ulipatikana karibu na mto zaidi ya wiki moja baada ya
kuonekana akibebwa na kuingizwa katika gari moja lisilo na nambari za usajili
katika mji wa Eldoret,umbali wa kilomita 200.
Bwana Yebei alitarajiwa kusafiri kuelekea mjini Hague kwa
kesi dhidi ya bwana Ruto-makamu wa rais
ambaye anakabiliwa na mashtaka
yanayohusiana na mashambulizi dhidi ya watu wa jamii ya kikuyu katika makaazi
ya wakalenjin huko Rift valley wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi miaka saba
iliopita.
No comments:
Post a Comment