Licha ya kuwa Diamond Platnumz hakuongozana na mpenzi wake
Zari The Boss Lady kwenda Nigeria Jumatatu hii, lakini kuna uwezekano mkubwa
wawili hao wakawa pamoja kwenye hafla ya ugawaji tuzo za michezo za Glo-CAF
Awards itakayofanyika Alhamisi Jan 8 jijini Lagos, ambapo Platnumz ni miongoni
mwa wasanii watakaotumbuiza.
Zari The Boss Lady amepost picha (hapo juu) asubuhi ya leo
Jumatano (Jan 7) akiwa kwenye ndege na kuandika “Another day, another flight.
Stay blessed”, inayoashiria kuna uwezekano mkubwa akawa anaenda kwa baby wake
Nigeria.
Diamond naye jana alipost picha zake mwenyewe (hapo juu)
akiwa anaonekana mpweke na kuandika, “Kuna mtu alikuwa mnyooonge na mpweke
jana…” hii inamaanisha mtu muhimu ambaye ni baby wake
ndiye anayekosekana.
Baada ya kuwa pamoja Uganda kwenye party ya Zari mwishoni
mwa mwaka jana, Zari na Diamond walisafiri pamoja kwenda Burundi na Rwanda na
ndio sababu kuna kila dalili pia watakua pamoja Nigeria licha ya kuwa
hawakusafiri pamoja.
No comments:
Post a Comment