Watu wazima hawana muda wa tendo la ndoa hali inayosababisha
kupungua kwa idadi ya watu Japan
Asilimia 50 ya watu wazima nchini Japan hawashiriki katika
tendo la ngono kulingana na utafiti, swala linalosababisha kupungua kwa idadi
ya watu nchini humo.
Ripoti hiyo iliofanywa na shirika la upangaji uzazi nchini
humo imebaini kwamba asilimia 49.3 ya watu 3000 waliohojiwa hawakushiriki ngono
mwezi uliopita.
Kati ya asilimia 48.3 waliohojiwa walisema kuwa
hawakushiriki katika ngono kwa mwezi moja huku asilimia 50.1 ya wanawake
wakijizuia kushiriki ngono.Takwimu zote zilipanda kwa asilimia 5 kutoka kwa ufatiti
uliofanywa awali mwaka 2012.
Walipoulizwa ni kwa nini hawashiriki katika tendo la ngono,
asilimia 21.3 ya wanaume walio katika ndoa walidai kuchoka baada ya kutoka
kazini huku asilimia 15.7 wakisema kuwa hawana haja ya kushiriki katika tendo
la ngono baad ya wake zao kujifungua.
Kati ya wanawake asilimia 23.8 walisema kuwa tendo la ngono
linasumbua na asilimia 17.8 wakidai walikuwa wamechoka.
Swala jengine la kushangaza ni kuongezeka kwa idadi ya
vijana ambao hawana hamu na tendo la ngono.Zaidi ya asilimia 20 ya wanaume
walio kati ya umri wa miaka 25 na 29 hakuwa na hamu ya kufanya ngono.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment