Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, April 11, 2015

IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI NNE



Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Zlatan Ibrahimovic amefungiwa kucheza mechi nne za ligi kuu ya Ufaransa baada ya kunaswa na picha za televisheni akitukana.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Sweden alikasirika na kuwashutumu waamuzi na pia kutukana baada ya timu yake kupoteza 3-2 dhidi ya 
 
Bordeaux mwezi uliopita. Ibrahimovic, 33, baadaye aliomba radhi na kusema matamshi yake "hayakuwa yamelenga Ufaransa au wananchi wake".
Atakosa mechi nne kati ya saba zilizosalia za ligi. Kamati ya nidhamu ilisema adhabu hiyo imezingatia "aina ya kosa na uzito wa matamshi yake".
Ibrahimovic pia atakosa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Barcelona kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea. Hata hivyo ataweza kucheza mechi ya fainali ya kombe la ligi siku ya Jumamosi dhidi ya Bastia.

No comments:

Post a Comment