Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, May 18, 2015

MANE AVUNJA REKODI YA HAT TRICK



Sadio Mane, wa Southampton amevunja rekodi ya kupachika mabao matatu - Hat trick - katika muda mfupi zaidi katika Ligi Kuu ya England. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Senegal amepachika mabao matatu- chini ya dakika tatu na kuweka rekodi mpya ya EPL.
Mane amefunga hat trick hiyo katika muda wa dakika mbili na sekunde 56 katika mchezo dhidi ya Aston Villa.
 
Mane amevunjilia mbali rekodi iliyowekwa na Robbie Fowler miaka 20 iliyopita. Fowler akiichezea Liverpool alifunga mabao matatu katika muda wa dakika nne na sekunde 33, kwenye mchezo dhidi ya Arsenal, Agosti 28 mwaka 1994.

No comments:

Post a Comment